• HABARI MPYA

    Monday, August 20, 2012

    YANGA WAANZA NA NNE BILA, TEGETE AJIKUMBUSHA KUFUNGA

    Wachezaji wa Yanga wakimpongeza Msuva
    David Luhende akisikitika baada ya kukosa bao la wazi


    Luhende anatoa krosi

    Hamisi Kiiza kulia

    Hatari langoni mwa Lyon

    Hatari langoni mwa Lyon

    Luhende akitafuta mbinu za kumtoka mtu

    Luhende amekwishamtoka mtu anachanga mbuga

    Kiungo wa Lyon, Adam Kingwande akiondosha mpira miguuni mwa Haruna Niyonzima

    Niyonzima akilalamika baada ya kudondoshwa

    Kingwande chini naye

    Semmy Kessi kushoto amekwishamtupa mtu chini, Msuva kulia na kilichofuata ni penalti 

    Msuva akiinuka baada ya kuangushwa na Kessy

    11 wa Yanga walioanza leo

    11 wa Lyon walioanza leo

    Msuva akishangilia bao
     Na Mahmoud Zubeiry
    YANGA SC imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Africfan Lyon, zote za Dar es Salaam katika mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Yanga ilitumia mchezo huo kuwapima wachezaji wake kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu na haukuwa mwanzo mbaya, timu ikicheza kwa utulivu na hata kuhimili vishindo vya wapinzani.
    Didier Kavumbangu, mshambuliaji mpya wa klabu hiyo aliyesajiliwa kutoka Atletico Olympique ya Burundi, alikuwa wa kwanza kuwainua vitini mashabiki wa Yanga dakika ya sita baada ya kupiga mpira ambao beki alipojaribu kuokoa ulimgonga kipa wake na kuingia nyavuni.
    Hadi mapumziko, Yanga walikuwa mbele kwa bao hilo 1-0 na kipindi cha pili, Haruna Niyonzima aliifungia Yanga bao la pili kwa penalti dakika ya 57, baada ya Simon Msuva kuchezewa rafu na Semmy Kessy kwenye eneo la hatari.
    Frank Damayo aliyeingia kuchukua nafasi ya Athumani Iddi ‘Chuji’ kipindi cha pili alitoa pasi nzuri kwa Simon Msuva ambaye aliifungia Yanga bao la tatu dakika ya 72, kabla ya Jerry Tegete kufunga la nne dakika ya 90+1.   
    Baada ya mchezo huu, Yanga ambao ni mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame inatarajiwa kuondoka Dar es Salaam Jumatano kwenda Kigali, Rwanda ambako itaweka kambi ya wiki mbili kujiandaa na Ligi Kuu.
    Ikiwa huko, Yanga itacheza mechi kadhaa za kujipima nguvu na vigogo wa Rwanda, kama APR, Rayon, Atracao na Polisi kabla ya kurejea Dar ves Salaam kuanza maandalizi ya Ligi Kuu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA WAANZA NA NNE BILA, TEGETE AJIKUMBUSHA KUFUNGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top