• HABARI MPYA

    Tuesday, August 21, 2012

    SHAURI AMTWANGA KO MGANDA, ATWAA TAJI LA IBF AFRIKA

    Girish Khetia wa Bidco Oil Limited (kulia), akimvalisha Shauri mkanda wa ubingwa wa IBF Afrika, baada ya kumpiga Kizito (kulia)

    Na Mahmoud Zubeiry
    BONDIA Ramadhan Shauri wa Tanzania, usiku huu amefanikiwa kutwaa ubingwa wa Afrika wa Shirikisho la Ndondi la Kimataifa (IBF), baada ya kumpiga kwa Technical Knockout (TKO) raundi ya nane, Sunday Kizito wa Uganda katika pambano lililokuwa la raundi 12, ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
    Baada ya kuokolewa kwa kengele kufuatia kipigo kikali kuanzia raundi ya saba, Kizito aliporejea kwenye kona yake ya bluu, alifikia kuangukia magoti, akishindwa kujimudu hadi aliposaidiwa na wasaidizi wake ambao walimuinua mikono juu kuashiria hawezi kuendelea na pambano.
    Awali, Kizito alionyesha upinzani mkali kwa Mtanzania huyo kuanzia raundi ya kwanza hadi ya nne, lakini taratibu mambo yalianza kumgeukia kuanzia raundi ya tano. Mikono miepesi ya Shauri iliyokuwa ikichomoka kwa haraka na kutua kwenye kichwa cha Kizito, ilikwenda ikimlainisha taratibu Mganda huyo na kufikia raundi ya nane, haikuwa ajabu alipotandikwa kama begi.
    Shauri alipigana kwa kiwango cha juu na kuashiria kwamba, taifa limempata shujaa mpya wa ndondi wa uzito wa Feather ambaye anaweza kufanya makubwa, kama atapewa sapoti ya kutosha.
    Pambano hilo liloandaliwa na Kitwe Promotions na kudhaminiwa na Bidco Oil Limited, chini ya usimamizi wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) lilitanguliwa na mapambano mengine kadhaa na Mtanzania mwingine, Nassib Ramadhan alimpiga kwa TKO raundi ya kwanza, dakika ya kwanza sekunde ya 40, Mkenya Isaac Odhiambo katika pambano la uzito wa Super Fly, lililokuwa la raundi nane.
    Ramadhani Mashudu alimpiga Ramadhani Mkundi kwa pointi za majaji wote watatu, katika pambano la raundi sita uzito wa Bantam, wakati Yonas Segere alimpiga kwa pointi za majaji wawili kwa mmoja, Seba Temba katika uzito wa Super Light, raundi sita pia na Bakari Mohamed alimpiga Bakari Maulid kwa pointi za majaji wawili kwa mmoja, uzito wa Feather, raundi nne.
    Kwenye ukumbi wa Chuo cha Uhasibu, Kurasini, lilifanyika pambano lingine la uzito juu na Alphonce Mchumia Tumbo alimtandika TKO, raundi ya kwanza, dakika ya kwanza sekunde ua 49, David Mrope ‘Zola D’.     
    Meza kuu

    Bondia Mada Maugo kulia akiwa na mwanamuziki Lady Maureen kutoka Kenya

    Girish Khetia kulia na Rais wa TPBC, Onesmo Ngowi

    Yonas Segere kushoto na Seba Temba

    Ramadhani Mashudu kushoto na Ramadhani Mkundi

    Ramadhani Mashudu kushoto na Ramadhan Mkundi

    Nassib Ramadhani kulia na Isaac Odhiambo

    Odhiambo akijikusanya kuinuka baada ya kukalishwa chini na konde la Nassib

    Promota Rutta wa Kitwe kushoto na Khetia

    Jaji Boniphace Wambura 

    Shauri kushoto






















    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SHAURI AMTWANGA KO MGANDA, ATWAA TAJI LA IBF AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top