| Mbwana Ally Samatta, mshambuliaji chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, leo anatarajiwa kuiongozxa klabu yake, TP Mazembe katika mchezo wa kwanza wa mzunguko wa pili wa Kundi B, Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zamalek mjini Cairo, Misri. Mazembe inashika nafasi ya pili kwenye kundi hilo kwa pointi zake nne, nyuma ya vinara, Al Ahly wenye pointi tisa na inahitaji lazima kushinda ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kuingia Nusu Fainali na kufufua matumaini ya kutwaa taji la tano. Berekum Chelsea ya Ghana pia ina pointi nne, ingawa inazidiwa wastani wa mabao na Mazembe na leo nayo itakuwa mwenyeji wa Al Ahly. |
0 comments:
Post a Comment