Tetesi za J'pili magazeti ya Ulaya


MODRIC AIKATAA TENA CHELSEA, YEYE NA REAL MADRID TU

Luka Modric, mwenye umri wa miaka 26, anajiandaa kuipiga chini ofa mpya ya Chelsea na kuhamia Real Madrid wiki hii.
Adam Johnson anajiandaa kuondoka Man City na kurudi nyumbani kwao, Kaskazini Mashariki, na Sunderland iko tayari kutoa pauni Milioni 10kwa ajili ya winga huyo wa England.
Adam Johnson
Sunderland inamtaka kiungo wa Man City, nyota wa zamani wa Middlesbrough, Adam Johnson
Roberto Mancini haridhiswhi na usajili wa pauni Milioni 12 wa Jack Rodwell kutoka Everton na bado anashangazwa na usajili wa Man City safari hii.
Andre Villas-Boas anatumai kusajili mshambuliaji mwingine mpya kabla ya kumalizika kwa wiki hii.
Newcastle haina tatizo na ofa za kuwakata wachezaji wake Cheick Tiote na Yohan Cabaye, kutoka Chelsea na Manchester United, ambazo zote zinawataka viungo hao.

FERGUSON AMEBAKIZA MIAKA MIWILI 

Sir Alex Ferguson anataka kustaafu ndani ya miaka miwili, baada ya kutengeneza timu mpya, inayoongozwa na Wayne Rooney na Robin van Persie.
Arsene Wenger amesema kwamba hajui kama winga wake Theo Walcott atasaini mkataba wa kuendelea kuichezea Arsenal.
Roberto di Matteo anatimai kiungo wake mkongwe, mwenye umri wa miaka 34, Frank Lampard atasaini mkataba mpya na klabu yake ya sasa, Chelsea.

MAN CITY WALITOA OFA KWA MESSI, IKAPIGWA CHINI...

Kitabu kipya kinasema kwamba, Manchester City "kwa bahati mbaya" ilitoa ofa ya kumsajili Lionel Messi, lakini kiulaini ikakataliwa, katika usiku ambao klabu hiyo ilichukuliwa rasmi na Sheikh Mansour mwaka 2008.