Tetesi za Ijumaa magazeti Ulaya
NURI SAHIN AAMUA KUTUA ARSENAL, AKATAA KUPELEKWA LIVERPOOL FC
Kiungo wa Real Madrid, Nuri Sahin, mwenye umri wa miaka 23, ametaka mpango wa kupelekwa kwa mkopo Liverpool usitishwe na badala yake apelekwe Arsenal, ambayo nyota huyo wa zamani wa Dortmund anatumaini itamsaidia kung'ara kutokana na kucheza Ligi ya Mabingwa.
Liverpool inataka kumsajli ama mmoja kati ya wachezaji wawili wa Spurs Steven Caulker au Michael Dawson, ikiwa beki Daniel Agger atahamia Manchester City.
Tottenham iko tayari kumsajili kiungo wa Chelsea, Raul Meireles, mwenye umri wa miaka 29, kama mbadala wa mchezaji anayetaka kuhamia Real Madrid, Luka Modric.
Mshambuliaji wa Arsenal, Nicklas Bendtner amesistiza msimamo wake wa kutaka kuihama klabu hiyo, akisema kwamba hatakuwa na furaha hadi afanye hivyo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, msimu uliopita alicheza kwa mkopo Sunderland, lakini hajafanikiwa kuhamishwa moja kwa moja.
Fulham imefufua nia yake ya kumsajili kiungo wa Blackburn, Steven N'Zonzi, mwenye umri wa miaka 23, ambaye hayuko kwenye mipango ya Steve Kean, baada ya kugoma kuichezea klabu hiyo msimu uliopita.
Mabingwa wa Urusi, Zenit St Petersburg wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester United, Dimitar Berbatov. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31 wa Bulgaria, amekwishaambiwa anaweza kuondoka Old Trafford.
AZMA KUU YA LIVERPOOL
Beki wa Liverpool, Jamie Carragher amesema kumaliza ndani ya Top-Four, kuliko kushinda Kombe lingine tofauti na Ligi Kuu, ndio azma kuu ya Liverpool msimu huu.
VAN PERSIE KWENYE MITANDAO
Uhamisho wa Robin van Persie kutoka Arsenal kwenda Manchester United umetawala utani katika mitandao.



.png)
0 comments:
Post a Comment