• HABARI MPYA

    Saturday, August 18, 2012

    MBUYU TWITE SASA YANGA...

    Mbuyu akisaini Yanga mjini Kigali mbele ya Bin Kleb

    Na Princess Asia
    BEKI mpya wa Yanga, Mbuyu Twite sasa huenda atajiunga na timu ikiwa Kigali, Rwanda wakati wa kambi ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Habari za kutoka ndani zimesema kwamba, mpango wa klabu hiyo ulikuwa ni kutaka Mbuyu aje kwanza Dar es Salaam wanachama na wapenzi wa timu hiyo wamuone ndipo aende na wenzake Kigali, lakini huenda hilo lisiwezekane.
    Kwa nini? Imeelezwa desturi ya Mbuyu anapoondoka kwao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwenda nje ya nchi yao kucheza soka huwa anamaliza hata mwaka bila kurejea kusalimia familia yake.
    Kwa sababu hiyo, baada ya kuchukua ‘faranga’ za Yanga, Mbuyu yuko na familia yake DRC hivi sasa akipewa Baraka kabla ya kuja kuanza maisha mapya Tanzania Bara.
    Yanga inatarajiwa kuondoka Dar es Salaam Jumatano ijayo kwenda Rwanda kuweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya, itakayohusisha pia na michezo ya kirafiki dhidi ya vigogo wa huko kama APR, Rayon, Atracao na Polisi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MBUYU TWITE SASA YANGA... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top