MFUMO wa kompyuta ulioletwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ndio utakaotoa hukumu dhidi ya beki Kelvin Yondani kuchezea Simba au Yanga. Habari za kuaminika kutoka ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) zinaeleza kuwa mfumo huo ni kati ya mabadiliko makubwa yaliyofanywa na CAF katika kusimamia soka la barani Afrika. TFF imepanga kuanzia kesho Jumatano hadi Ijumaa kupitia pingamizi na majina ya timu mbalimbali zilizowasilisha majina kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Timu mbili zenye upinzani wa jadi za Simba na Yanga kila moja imewasilisha jina la Yondani kwa TFF kwa ajili ya kuichezea timu hiyo. Yanga ilimsainisha mchezaji huyo Juni, mwaka huu kama mchezaji huru wakati alipokuwa kwenye kambi ya Taifa Stars iliyokuwa inajiandaa na mechi za michuano ya awali ya Kombe la Dunia. Simba ilijibu mapigo kwa kudai ni mchezaji wao halali na kupeleka mkataba wake Juni 10, mwaka huu huko TFF. Timu hiyo, hata hivyo, iliboronga kwenye mkataba wake iliyoongeza na Yondani kwani ulionyesha ulikuwa unatakiwa kuanza Desemba 12, 2012 wakati Yondani alimaliza mkataba wake mwishoni mwa Mei, mwaka huu. Klabu zote za Ligi kuu zimepewa kanda maalumu zilizotolewa na CAF, ambazo zinatakiwa kuwekwa habari za wachezaji waliosajiliwa na timu mbalimbali. "Timu zote zinatakiwa kuweka maelezo ya historia kuanzia akiwa yosso ili kufahamu mathalani timu gani inatakiwa kulipwa fidia. Pia wanatakiwa kujaza habari za mkataba wake," kilieleza chanzo cha kuaminika ndani ya TFF. Habari zaidi zinaeleza kuwa baada ya CD zile kujazwa taarifa za wachezaji ndio zilipelekwa TFF. TFF wanatakiwa kuzichapa taarifa za wachezaji kutoka katika CD hizo na kuzikagua kwa kutumia mashine kama inavyofanyika kwenye pasi za kusafiria watu wanapopita katika viwanja vya ndege. "Tukipitisha karatasi ile kwenye mashine zetu basi itabaini kama kuna tatizo katika usajili wa timu yoyote. Kama watu wa Uhamiaji wanavyofanya kwa wasafiri kwenye uwanja wa ndege wakati wa ukaguzi wa pasi za kusafiria na tiketi," kiliongeza chanzo hicho. Kutokana na mfumo huo, inaaminika Kamati ya Katiba, Sheria na Haki za Wachezaji haitakuwa na kibarua kigumu kuamua suala la Yondani kwani mashine tu zitafanya kazi. Taarifa zitakazotolewa na kompyuta ndio zitaamua hatma ya Yondani na kukata mzizi wa fitina wa suala hilo ambalo limetikisa medani ya soka nchini. Wadau wa soka wanasubiri kuona Yondani ataidhinishwa timu ipi kutokana na mvutano huo wa Simba na Yanga. Yanga, hata hivyo, inaelekea ina nafasi kubwa ya kumnyaka beki huyo kwani TFF ilitoa baraka zake kwa Yondani kuchezea Yanga kwenye Kombe la Kagame. TFF ilijitetea kuwa iliangalia mkataba wake na Yanga na ikazingatia kuwa mashindano ya Kagame hayakuwa na kanuni kali za usajili na ndiyo maana hata Selemani Kassim Selembe aliruhusiwa kuchezea Mafunzo ya Zanzibar wakati alikuwa kwenye mipango ya kujiunga na Coastal Union ya Tanga. Mfumo huo wa usajili, ni sehemu ya mabadiliko yaliyofanywa na CAF, ambayo inataka timu kuwasilisha taarifa za mikataba au umiliki viwanja vyao vya kuchezea na vile vya mazoezi. Vigezo hivyo ndio vinatakiwa kutekelezwa na timu ili kushiriki katika mashindano ya Afrika. SOURCE: Gazeti la Mwanaspoti |
How to make the perfect custard creams – recipe
-
They may be pennies a packet, but the ubiquitous custard cream can be a
revelation if you make them at home. But who has come up with the ideal
bake?
28 minutes ago


.png)
0 comments:
Post a Comment