Tetesi za J'tatu magazeti ya Ulaya


KAKA KUTUA MANCHESTER UNITED, SONG HUYOO CAMP NOU
Kaka
Kaka anaweza kuhamia Ligi Kuu England 
Kiungo wa kimataifa wa Brazil, mwenye umri wa miaka 30, Kaka amepewa ofa ya kwenda kucheza kwa mkopo wa muda mrefu Manchester United, wakati Real Madrid ikijiandaa kumpokea Luka Modric.
Manchester City imejiunga kwenye mbio moja na Chelsea za kuwania saini ya mshambuliaji wa Fiorentina, Stevan Jovetic aliyezaliwa miaka 22 iliyopita.
Sunderland imeweka dau la pauni Milioni 10m kwa ajili ya kiungo wa Manchester City, Adam Johnson.
Roberto Martinez amesema taarifa za uhamisho wa Victor Moses, mwenye umri wa miaka 21, kwenda Chelsea bado zipo mbali na ukweli.
Daniel Agger, mwenye umri wa miaka 27, yu tayari kusaini mkataba mpya na Liverpool na 'kuitolea mbavuni' Manchester City - licha ya kulimwa kadi nyekundu katika mechi ya ufunguzi ya Ligi Kuu ya England dhidi ya West Brom.

WENGER AMUUZA PAUNI MILIONI 15 SONG

Alex Song
Arsene Wenger amekubali yaishe kwa Alex Song, anaondoka
Arsene Wenger ametaka pauni Milioni 15 kumuuza Alex Song kwenda Barcelona, baada ya kiungo huyo aliyezaliwa miaka 24 iliyopita kuonyesha wazi anataka kuhamia Camp Nou.
Manager Roberto Mancini ametakiwa na wamiliki wa Manchester City, wa Abu Dhabi kuacha mashambulizi yake kwa Mkurugenzi wao wa Michezo, Brian Marwood.

TATE AKOMA NA LAUDRUP

Beki wa Swansea City, Alan Tate amesema kocha mpya Michael Laudrup bado ni mchezaji mzuri mazoezini - ingawa ana umri wa miaka 48.