![]() |
Yanga |
Na Mahmoud Zubeiry
MABINGWA wa soka Afrika Mashariki na Kati, Yanga SC ya Dar es Salaam, leo wanatarajiwa kushuka dimbani kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kumenyana na African Lyon katika mchezo wa kirafiki, ambao imeelezwa beki Mbuyu Twite kutoka APR ya Rwanda atacheza.
Lakini mbaya zaidi hadi asubuhi hii, beki huyo alikuwa hajawasili nchini, ingawa BIN ZUBEIRY ilipowasiliana na kiongozi mmoja wa klabu hiyo, alisema ‘Shaka ondoa, utamuona Twite uwanjani leo’.
Huo utakuwa mchezo wa kwanza wa kirafiki kwa Yanga, tangu itwae ubingwa wa Kombe la Kagame mwezi uliopita na kwa wakati huo imekuwa ikijifua tu kwenye Uwanja wa sekondari ya Loyola, Mabibo, Dar es Salaam.
Mbali na Twite, mashabiki wa Yanga leo pia watapata fursa ya kumshuhudia kwa mara ya kwanza, mshambuliaji Didier Kavumbangu waliyemsajili kutoka Atletico Olimpique ya Burundi.
Kavumbangu ndiye aliyewafunga Yanga mabao yote mawili, walipomenyana na timu hiyo ya Burundi na kulala 2-0 na kwa kuwa mfungaji bora wa Kagame, Said Bahanuzi ‘Spider Man’ ni mgonjwa, Didier lazima ataanza.
Tayari Yanga imewasilisha usajili wake Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), hivyo kocha Tom Saintfiet raia wa Ubelgiji anaweza kumpanga yeyote atakaye.
Kikosi kamili cha Yanga ni; Makipa; Yaw Berko, Ally Mustafa ‘Barthez’ na Said Mohamed.
Mabeki; Shadrack Nsajigwa (Nahodha), Godfrey Taita, Juma Abdul, Oscar Joshua, David Luhende na Stephano Mwasika, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Mbuyu Twite, Ibrahim Job na Ladislaus Mbogo.
Viungo; Athuman Idd ‘Chuji’, Juma Seif ‘Kijiko’ na Salum Telela, Nizar Khalfan, Shamte Ally, Idrisa Rashid, Omega Seme, Haruna Niyonzima, Rashid Gumbo na Nurdin Bakari.
Washambuliaji; Said Bhanaunzi ‘Spider Man’, Hamisi Kiiza ‘Diego’, Didier Kavambagu na Jerry Tegete.
Kiungo Frank Domayo na mshambuliaji Simon Msuva, wanaendelea kukomazwa katika kikosi cha kwanza, wakitokea kikosi cha pili.
Awali, Yanga ilikuwa icheze Coastal Union leo, lakini Meneja wa Yanga, Hafidh Suleiman amesema mechi hiyo imefutwa na sasa wanacheza na Lyon.
Awali, Yanga ilikuwa icheze Coastal Union leo, lakini Meneja wa Yanga, Hafidh Suleiman amesema mechi hiyo imefutwa na sasa wanacheza na Lyon.
0 comments:
Post a Comment