EMMANUEL ADEBAYOR anatumai
kukamilisha uhamisho wa pauni Milioni 5, kutua moja kwa moja Spurs wiki hii.
Makubaliano yalikwishafikiwa
baina ya Manchester City na klabu hiyo ya White Hart Lane, zaidi ya wiki sita
zilizopita, lakini yalikwama kutokana na Adebayor juu ya maslahi yake binafsi.
Lakini Adebayor sasa
ameonyesha yuko tayari kupokea mshahara wa chini, kutoka ule aliokuwa akipewa
awali katika mkataba wa City.
Mshambuliaji huyo wa
kimataifa wa Togo, amebakiza miaka miwili kwenye mkataba wake wa mshahara wa
pauni 170,000 kwa wiki, aliosaini akijiunga na City mwaka 2009 kutoka Asrenal.
Mabingwa City watapata
hasara kwa mchezaji huyo waliyemnunua pauni Milioni 25 kutoka Arsenal. Kocha Mtaliano,
Roberto Mancini alisema hivi karibuni: “Samahani kwa Adebayor, kwa sababu ni
mchezaji mzuri. Hakuna nafasi kwa yeye kucheza kwetu, hivyo kwa sababu hiyo, ni
muhimu tumepata suluhisho.”
SOURCE: http://www.thesun.co.uk
0 comments:
Post a Comment