• HABARI MPYA

    Tuesday, April 17, 2012

    YANGA WAINGIZA MILIONI 15, WAAMBULIA MILIONI 2

    Yanga SC
    MCHEZO wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Toto Africans na Yanga iliyochezwa juzi (Aprili 15 mwaka huu) kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ilishuhudiwa na watazamaji 7,186 na kuingiza sh. 15,392,000.
    Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura ameiambia bongostaz.blogspot.com mchana huu kwamba viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000 kwa jukwaa kuu na sh. 2,000 mzunguko.
    Wambura amesema kwamba baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 2,347,932 kila klabu ilipata sh. 2,729,060, uwanja sh. 909,686.
    TFF imepata Sh. 909,686, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA) sh. 363,874, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 454,843, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 90,968 na asilimia 10 ya gharama za mechi ni sh. 909,686.
    Gharama za awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000. Mwamuzi wa akiba sh. 30,000, posho ya kujikimu kwa kamishna na waamuzi sh. 160,000, gharama ya tiketi sh. 2,300,000.
    Gharama nyingine ni Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila tiketi; kila klabu ilipata sh. 503,020 wakati Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA) kilipata sh. 431,160.
    Wakati huo huo: Wambura amesema kwamba Chama Soka Mtwara (MTWAREFA) kimepata viongozi wapya katika uchaguzi uliofanyika juzi (Aprili 15 mwaka huu) ukumbi wa Clinical Officers Training College wilayani Masasi.
    Waliochaguliwa ni Athumani Kambi (Mwenyekiti), Vincent Majili (Katibu Mkuu), Kazito Mbano (Mhazini) na mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Fredrick Nachinuku.
    Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa MTWAREFA walikuwa 30 ambapo Kambi alipata kura 23 za ndiyo na saba za hapana wakati Majili alipata kura 27 dhidi ya tatu za Charles Haule.
    Nafasi nyingine hazikuwa na wagombea ambapo uchaguzi mdogo utaitishwa baadaye.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA WAINGIZA MILIONI 15, WAAMBULIA MILIONI 2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top