• HABARI MPYA

    Wednesday, June 06, 2012

    KIFAA KINGINE SIMBA SC KUSAINI KESHO YANGA

    KIFAA kingine cha Simba kimeomba kusajiliwa Yanga kikidai hakina mkataba na klabu yake ya sasa, kwani kilisaini mkataba wa mwaka mmoja, ambao umemalizika.
    Lakini Abdallah Bin Kleb, Mgombea Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga katika uchaguzi wa Julai 15, mwaka huu amemuambia mchezaji huyo kwamba awape ushahidi wa kutosha, ili wajiridhishe na watamsaini kwa sababu wanaheshimu soka yake.
    Kesho, mchezaji huyo fundi, aliye kambini timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars- ameahidi kupeleka ushahidi ili naye ajichotee noti zenye alama ya mnyama tembo kama alizokusanya Yondan usiku huu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIFAA KINGINE SIMBA SC KUSAINI KESHO YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top