• HABARI MPYA

    Monday, August 01, 2016

    NI NAMIBIA MABINGWA WA COSAFA U-17

    TIMU ya Namibia imetwaa ubingwa wa vijana chini ya umri wa miaka 17 kwa nchi za kusini mwa Afrika, maarufu COSAFA baada ya ushindi wa penalti 3-1 dhidi ya Afrika Kusini kufuatia sare ya 1-1 nchini Mauritius jana.
    Namibia iliyofungwa 4-0 na Afrika Kusini katika makundi, lakini ilionyesha mabadiliko makubwa katika fainali hadi kutwaa ubingwa kwa matuta.
    Baada ya kipindi cha kwanza kumalizika kwa sare ya bila mabao, Namibia ilifanikiwa kupata bao la kuongoza kupitia kwa Godwin Awaseb aliyefunga baada ya dakika tatu tu tangu aingie kutokea benchi, kabla ya Thabiso Monyane kuisawazishia Afrika Kusini.
    Katika mchezo uliotangulia wa kusaka mshindi wa tatu, Malawi iliichaopa 2-0 Kenya mabao ya Peter Banda na Francisco Madinga.

    TAKWIMU MUHIMU ZA COSAFA 2016:
    Mshindi wa tatu; Kenya 0 Malawi 2 
    Faiali; Afrika Kusini 1 - Namibia 1
    WAFUNGAJI WA MABAIO:
    5 – Peter Banda (Malawi)
    4 – Abram Tjahikika (Namibia)
    3 – Eldery Morgan (Namibia), Nicholas Mulilo (Zambia)
    2 – Franck Chizuze (Malawi), Damiano Kola (Zambia), Luke le Roux (Afrika Kusini), Francisco Madinga (Malawi), Linamandla Mchilizeli (Afrika Kusini), James Monyane (Afrika Kuini), Fabrizio Mosa (Madagascar), Kenneth Mukuria (Kenya), Siphamandla Ntuli (Afrika Kusini), George Nyimbili (Zambia)
    1 – Godwin Awaseb (Namibia), Raphael Banda (Malawi), Bonga Dladla (Afrika Kusini), Neehal Hurdoyal (Mauritius), Mathiot Juninho (Shelisheli), Rivaldo Laksman (Namibia), Mswati Mavuso (Afrika Kusini), Mjabulise Mkhize (Afrika Kusini), Matteo Monple (Mauritius), Kunda Nkandu (Zambia), Benjamin Phiri (Zambia), Tyreese Pillay (South Africa), Mwiza Siwale (Zambia)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NI NAMIBIA MABINGWA WA COSAFA U-17 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top