• HABARI MPYA

    Wednesday, June 08, 2016

    MALINZI AWAFARIJI WANIGERIA MSIBA WA KESHI

    RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa Kocha Mkuu wa zamani wa Nigeria, Stephen Okechukwu Keshi (pichani kulia) kilichotokea ghafla leo Juni 08, 2016 kwa mujibu wa vyombo vya habari vya kimataifa.
    Kutokana na kifo hicho, Rais Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa Shirikisho la Soka Nigeria (NFF), Amaju Pinnick, familia ya marehemu Keshi pamoja na ndugu, jamaa, marafiki walioguswa na msiba huo wa gwiji huyo aliyepata kuwa nahodha wa kikosi cha Taifa Nigeria ‘Super Eagles’.
    Katika rambirambi ambazo zimefika pia katika Ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa (FIFA), Rais Malinzi amesema kuwa japokuwa Keshi ametangulia mbele za haki, mchango wake kwenye mpira wa miguu hautasahaulika kwani atabaki kuwa alama ya maendeleo ya mchezo wa soka.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MALINZI AWAFARIJI WANIGERIA MSIBA WA KESHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top