MANCINI AWASILISHA OMBI LA RASMI LA KUSAJILIWA NEYMAR MAN CITY KWA PAUNI MILIONI 50

Roberto Mancini atamuomba Mkurugenzi mpya wa Michezo wa Manchester City, Txiki Begiristain kuandaa dau la pauni Milioni 50 kwa ajili ya kumsajili Mbrazil, Neymar, mwenye umri wa miaka 20, kutoka Santos msimu ujao.
Kiungo wa Ajax, Toby Alderweireld, mwenye umri wa miaka 23, aliyeripotiwa kuwaniwa na Tottenham na Newcastle United, ataruhusiwa kuondoka Januari iwapo tu klabu hiyo ya Uholanzi itapata ada ya uhamisho baab kubwa, kwa mujibu wa kocha Frank De Boer.
Neymar
Neymar anaweza kuhamia Man City mwaka 2013
Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers amesema kwamba anasaka mkali mwenye kipaji cha kufunga mabao kwa ajili ya kumsajili Januari.
Na klabu hiyo ya Anfield ipo tayari kutoa pauni Milioni 6 kumsajili Klaas-Jan Huntelaar, mwenye umri wa miaka 29, baada ya kupata taarifa Mholanzi huyo amekataa kwa mara ya mwisho kuongeza mkataba na Schalke.
Manchester United haitaanza mazungumzo ya kuongeza mkataba na mkongwe wake mwenye umri wa miaka 39, Ryan Giggs hadi mwishoni mwa msimu.
Mshambuliaji wa Spurs, Emmanuel Adebayor, mwenye umri wa miaka 28, anatakiwa na Atletico Madrid, wakati klabu hiyo ya Hispania inataka achezea pamoja na mshambuliaji Radamel Falcao, anayetakiwa na Chelsea na klabu nyingine kadhaa Ulaya.

VAN PERSIE ASEMA HESHIMA YAKE KWA ARSENAL ILIMZUIA KUSHANGILIA BAO LAKE JANA

Robin van Persie amesema heshima yake kwa Arsenal ilimzuia kishangilia baada ya kuwafunga bao jana timu yake hiyo ya zamani, kwenye Uwanja wa Old Trafford akiichezea klabu yake ya sasa Manchester United, iliyoshinda 2-1.
Nyota wa zamani wa , Mikael Silvestre anaamini Jack Wilshere kuimarika kwake kwa kuwa fiti tena kutaisaidia klabu hiyo kumaliza ukame wa muda mrefu wa mataji katika Kombe la Ligi.
Baadhi ya mashabiki wa Arsenal walimzomea Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Ivan Gazidis, baada ya kumuona Van Persie akiifungia bao la kwanza Manchester United kwenye Uwanja wa Old Trafford jana.
Mchezaji wa Ajax, Christian Eriksen hajuti kukataa ofa ya kujiunga na Manchester City mwaka 2011. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 20 alifunga bao dhidi ya City msimu huu katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, akiiwezesha klabu yake ya Uholanzi kushinda.

DI CANIO AGEUKA MBOGO SWINDON

Kocha wa Swindon, Paulo Di Canio anataka kuwapiga faini wachezaji baada ya kutolewa kwenye Kombe la FA na amewaita wote mazoezini leo saa 1.30 asubuhi kujibu kwa nini watolewe na timu isiyoshiriki ligi yoyote, Macclesfield.