Dogo Aslay |
Na Princess Asia
MSANII chipukizi wa Bongo Fleva, Dogo Aslay kutoka kundi la
Wanaume Family TMK, ameteuliwa kuwania tuzo za muziki Afrika (KORA) kupitia
kipengele cha Msanii Bora Anayechipukia kutoka Afrika Mashariki.
Dogo huyo anayewakuna kuanzia watoto hadi wakubwa kwa nyimbo
zake ‘tamu’, ameingia kwenye kinyang’anyiro cha tuzo za KORA ambazo hutolewa
Afrika Kusini, kupitia wimbo wake wa Niwe
NaweI ambao ‘unabamba’ ile mbaya.
Meneja wea Kundi la Wanaume Family, Said Fela ameiambia BIN
ZUBEIRY mida hii kwamba Aslay amepokea kwa furaha kubwa matokeo hayo na
anawashukuru Watanzania kwa kuikubali kazi yake.
Fela amesema Asaly anawashukuru pia waandaaji wa tuzo hizo
kwa kuithamini kazi yake na kuiingiza katika orodha ya kazi bora Afrika, kwani
hiyo ni heshima kubwa kwake na kwa taifa lake.
Pamoja na hilo, Aslay ameomba Watanzania wafuatilie mchakato
wa tuzo hizo ili kujua namna ya kumpigia kura, hatimaye anyakue tuzo hiyo.
“Naomba wapenzi wa muziki nchini kwa ujumla wafuatilie
mchakato huo ili waweze kumpa sapoti Dogo abebe tuzo hiyo na kuzidi kuitangaza
Tanzania katika medani ya kimataifa ya muziki,”alisema Fela.