Football | CAF Champions League
| |
Al Ahli take African Champions League
Hilo linakuwa taji la saba na kuifanya klabu hiyo ya Misri iendelee kuwa klabu iliyotwaa mara nyingi zaidi taji hilo.
Ahly imetwaa taji hilo kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2..
El Sayed Hamdi, alimtoka beki Walid Hichri na kuingia kwenye eneo la penalti akitokea wingi ya kushoto na kumsetia bao la ufunguzi Nagui dakika mbili kabla ya mapumziko.
Soliman alitengeneza 2-0 kwa shuti dhaifu ambalo mabeki wa Esperance walishindwa kuzia na tangu hapo mambo yakawa magumu kwao,kwani walitakiwa kushinda mabao matatu, lakini wapata moja la kufutia machozi lililotiwa kimiani na Yannick Ndjeng.