• HABARI MPYA

    Friday, August 17, 2012

    SIMBA YAFICHUA SIRI YA ARUSHA

    Kikosi cha Simba SC

    Na Princess Asia
    KLABU ya Simba imesema kwamba, imeweka kambi Arusha kwa sababu mbili kubwa, mosi wanaona wana bahati na mkoa huo na pili ni sehemu nzuri kwa mazoezi kutokana na hali yake ya hewa.
    Ofisa Habari wa mabingwa hao wa Ligi Kuu, Ezekiel Kamwaga alisema jana kwamba Arusha ni mkoa ambao una hali ya hewa ya baridi, hivyo wachezaji wanafanya mazoezi kwa muda mrefu bila kuchoka.
    “Kwa hiyo wakitoka huko na kurudi Dar es Salaam, wataweza kucheza vizuri sana wakiwa fiti kiasi cha kutosha kutokana na mazoezi mengi ya Arusha,”alisema.
    Aidha, Kamwaga alisema kwamba msimu uliopita Simba iliweka kambi Arusha pia na ikafanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu pamoja na kuwafunga wapinzani wao wa jadi, Yanga SC mabao 5-0.
    “Kwa hiyo mambo hayo mawili makubwa ndio yalitufanya tuweke tena kambi Arusha na tunaamini kabisa tutanga’ara kama msimu uliopita,”alisema.
    Kikosi cha Simba kinaendelea na mazoezi mjini Arusha kwa wiki mbili sasa chini ya kocha wake Mkuu, Mserbia Profesa Milovan Cirkovick na kitaanza msimu mpya kwa mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya washindi wa pili wa ligi hiyo, Azam FC.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA YAFICHUA SIRI YA ARUSHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top