• HABARI MPYA

    Sunday, August 19, 2012

    BIN ZUBEIRY NA FAMILIA YAKE WALIVYOSHEREHEKEA EID YAO LEO

    Baada ya sala ya Eid El Fitri, kwa pamoja na familia yangu, tulikwenda kujumuika na watoto (yatima) wa kituo cha New Home Family Group, kilichopo Mji Mwema Ungondoni, Kigamboni, Dar es Salaam.
    Tulikula pamoja, tukafurahia Eid yetu. Kwangu, kama mzazi nilifarajika kuwapa faraja watoto wa kituo hicho. Nilifarijika kuwapa watoto wangu somo fulani, katika umri mdogo. Nilifurahi jinsi walivyoonyesha upendo kwa watoto wenzao. Nilifurahi jinsi walivyoonyeshwa upendo na watoto wa kituo hicho.
    Mwanzoni, walikuwa kama waoga waoga, kwa sababu ni mara ya kwanza kwao kwenda kujumuika na watoto ambao hawafahamiani nao. Lakini kadiri walivyozidi kukaa pamoja, walizoeana na hata niliposema sasa inatosha tuondoke, nilihisi kama nawakatili.
    Watoto wangu na watoto wa kituo hicho walipenda kuendelea kuwa pamoja. Watoto wangu, wakaomba siku moja niwapeleke tena kwenye kituo hicho wakacheze na wenzao. Wote walipata marafiki.
    Kwa ujumla nilifurahi sana kutembelea kituo hicho chenye jumla ya watoto 35, ambacho bado kinahitaji misaada ili kiweze kuwahudumia vema watoto hao, kama ambavyo mmoja wa walimu wa kituo hicho, Michael Lugendo, alisema kwamba kwa sasa wanakabiliwa na changamoto ya choo.
    Choo chao ‘kimefurika’ kwa sababu kilitengenezwa vibaya na wanahitaji misaada ya fedha au vifaa vya ujenzi, ili wawewze kukikarabati kiwe katika hali nzuri na kuepuka kuhatarisha afya za watoto zaidi ya 35.
    Sote tunafahamu, chanzo kikubwa cha maradhi ya milipuko ni ukosefu wa choo bora- basi ipo haja kwa wenye uwezo kujitolea kusaidia changamoto hiyo inayowakabili watoto wetu wa New Hope Family Centre, Mji Mwema Ungondoni, Kigamboni.
    Naam, kwangu, mimi mtoto wa marehemu Alhaj Ramadhan Zubeiry, hivi ndivyo nilivyosherehekea Eid yangu na sasa maisha mengine yanaendelea kama kawaida. Eid Mubbarak.

    Watoto wakipakuliwa chakula

    Princess Asia akiwa na rafiki yake wa kituo hicho

    Prince Akbar akiwa na rafiki yake wa kituo hicho

    Precious akiwa na rafiki yake wa kituo hicho

    Prince Akbar wa pili kutoka kulia, akila na watoto wenzake wali ndondo 

    Princess Asia katikati kutoka, akila na watoto wenzake wali ndondo.

    Precious kushoto, akiwa na Princess Asia na mtoto wa kituo hicho wakipata wali ndondo

    Prince Akbar mwenye kanzu

    Katika picha ya pamoja, mimi na watoto wa kituo hicho 

    Mtoto Precious akikabidhi zawadi aliyowapelekea watoto wa kituo hicho kwa Bi Maimuna Mussa, mmoja wa walezi wa kituo hicho.

    Mtoto Princess Asia, akikabidhi zawadi aliyowapelekea watoto wa kituo hicho kwa Bi Maimuna Mussa

    Mtoto Prince Akbar akikabidhi zawadi aliyowapelekea watoto wa kituo hicho kwa Bi Maimuna Mussa

    Prince Akbar akikabidhi zawadi zaidi kwa mtoto mwenzake.

    Nikiwa na Michael Lugendo, ninawa tayari kwa chakula 

    Nikiwa na Michael Lugendo, tukipata chakula, huku tukijadiliana mambo

    Nikiwa na Michael Lugendo, tukipata chakula, huku tukijadiliana mambo

    Nikiwa na Michael Lugendo, tukipata chakula, huku tukijadiliana mambo

    Nikiwa na Michael Lugendo, tukipata chakula, huku tukijadiliana mambo

    Nikiwa na Michael Lugendo, tukipata chakula, huku tukijadiliana mambo

    Nikiwa na Michael Lugendo, tukipata chakula, huku tukijadiliana mambo

    Nikiwa na Michael Lugendo, tukipata chakula, huku tukijadiliana mambo

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BIN ZUBEIRY NA FAMILIA YAKE WALIVYOSHEREHEKEA EID YAO LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top