Tetesi za Ijumaa magazeti Ulaya

VAN PERSIE AWAFUKUZA EDIN DZEKO, CARLOS TEVEZ MAN CITY

KLABU ya Manchester City inajaribu kuwauza washambuliaji wake Carlos Tevez, Edin Dzeko, Emmanuel Adebayor na Roque Santa Cruz ili kuchanga fedha za kumsajili mpachika mabao wa Arsenal, Robin van Persie.
Gareth Bale
Gareth Bale 
WINGA wa Wales, Gareth Bale, mwenye umri wa miaka 22, anaweza kumfuata kocha Harry Redknapp kuondoka Tottenham, baada ya wakala wake kusema kukosa kwa klabu hiyo tiketi ya Ligi ya Mabingwa ni tatizo.
KLABU za Everton na Wolves zinaamini mchezaji zinayemuwania, Bjorn Bergmann Sigurdarson, mwenye umri wa miaka 21, hataruhusiwa na klabu yake, ingawa itamuumiza kwa sababu amedhamiria kuondoka.
KLABU ya Arsenal ina nia ya kumsajili kiungo wa kimataifa wa Urusi, Alan Dzagoev, mwenye umri wa miaka 21. Mchezaji huyo mwenye thamani ya pauni Milioni 13 wa CSKA Moscow, anamaliza mkataba wake Desemba.
MCHEZAJI anayewaniwa na klabu za Manchester United, Arsenal na Tottenham, Klaas-Jan Huntelaar, mwenyr umri wa miaka 28, anaweza kupatikana kwa dau la pauni Milioni 17, baada ya Meneja Mkuu wa Schalke, Horst Heldt kuthibitisha mshambuliaji huyo amewekwa sokoni.

ENGLAND WAONYWA

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Bolton, Johan Elmander, mwenye umri wa miaka 31, ameionya England kujiandaa na mchezo mgumu dhidi ya Sweden.

AVB KUTUA SPURS

Andre Villas-Boas
Andre Villas-Boas 
KOCHA wa zamani wa Chelsea, Andre Villas-Boas yumo kwenye orodha ya makocha wanaotakiwa na Tottenham kurithi mikoba ya Harry Redknapp, ambaye amefukuzwa Alhamisi.
KLABU ya Besiktas imempa ofa Alex McLeish arejee haraka katika menejimenti, kufuatia kumfukuzwa na Aston Villa mwezi uliopita.