Tetesi za Alhamisi magazeti Ulaya

CHELSEA KUNG'OA KIUNGO EVERTON

KLABU ya Chelsea inamtolea macho ikitaka kumsajili kwa dau la pauni Milioni 20, kiungo wa Everton mwenye umri wa miaka 24, Marouane Fellaini,.
KLABU ya Queens Park Rangersinataka kumsajili mshambuliaji wa Montpellier na Ufaransa, Olivier Giroud, mwenye umri wa miaka 25, ambaye thamani yake ni pauni Milioni 50.
Olivier Giroud
Giroud 
KLABU mpya Ligi Kuu, Southampton inajipanga kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Burnley, Jay Rodriguez, mwenye umri wa miaka 22, kwa dau la pauni milioni 7.
KOCHA Chris Hughton anapanga kurejea Birmingham City kumchukua beki Curtis Davies, mwenye umri wa miaka 27, mara atakapothibitishwa kocha mpya wa Norwich.
KLABU ya Arsenal ipo karibu kumsajili mshambuliaji wa Malaga, mwenye umri wa miaka 22, Salomon Randon nyota wa kimataifa wa Venezuela, ambaye imeripotiwa dau lake katika klabu hiyo ya Hispania ni pauni Milioni 20.
KLABU ya Liverpool inamtaka winga wa Manchester City, Adam Johnson, mwenye umri wa miaka 24, ikiwa tayari kutoa dau la pauni Milioni 16, na itampa uhakika wa kucheza katika kikosi cha kwanza.

NAHODHA WA BAADAYE ENGLAND

KIUNGO wa Sunderland, David Meyler amempendekeza Jordan Henderson kuwa Nahodha wa baadaye wa England.
KLABU ya Chelsea imemuambia Roberto Di Matteo ingependa kumuacha aendelee kuwa kocha na vyanzo vimesema kocha huyo atakuwa kazini Stamford Bridge mwanzoni mwa msimu mpya.