• HABARI MPYA

  Wednesday, June 08, 2016

  STEPHEN KESHI 'THE BIG BOSS' AFARIKI DUNIA LEO

  MCHEZAJI na kocha wa zamani wa Nigeria, Stephen Okechukwu Keshi 'The Big Boss' (pichani kulia) amefariki dunia mapema leo.
  Keshi aliyefiwa na mkewe mwenye umri wa miaka 33, Kate, mwaka jana alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya saratani na inadhaniwa kifo chake kimesababishwa na shinikizo la damu huko jimbo la Benin Edo.
  Kwa mujibu wa familia ya marehemu kocha huyo hakuonyesha dalili zozote za kuumwa kabla ya kifo chake. Ameacha watoto wanne na mama yake.
  Keshi, kocha pekee Mnigeria kuiwezesha Super Eagles kushinda Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2013 na kuweka rekodi ya mtu wa pili barani kushinda taji hilo kama mchezaji na baadaye kocha.
  Mtu mwingine aliyeweza kutwaa taji la AFCON kama mchezaji na baadaye kocha ni Mahmoud El-Gohary wa Misri.
  Keshi aliichezea Nigeria kuanzia mwaka 1982 akiwa ana umri wa miaka 20 hadi mwaka 1994 na muda mrefu alikuwa Nahodha wa Super Eagles na alifunga mabao muhimu akiwa beki wa kati.
  Pia amefundisha timu za taifa za Togo na Nigeria katika Kombe la Dunia pamoja na Mali. Mungu ampumzishe kwa amani gwiji wa soka Nigeria na Afrika.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: STEPHEN KESHI 'THE BIG BOSS' AFARIKI DUNIA LEO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top