• HABARI MPYA

    Monday, June 06, 2016

    DANTE LA MTIBWA SUGAR LADONDOKA JANGWANI MIAKA MIWILI

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    BEKI wa Mtibwa Sugar, Andrew Vincent 'Dante' (pichani kushoto) amesaini Mkataba wa miaka miwili kujiunga na Yanga SC leo hii.
    Vincent, mmoja wa mabeki wa kati waliofanya vizuri msimu huu amesaini muda mfupi baada ya kusiani kipa wa Prisons, Beno Kakolanya leo. 
    Dante sasa anakwenda kupambana kugombea namba dhidi ya mabeki wengine wa kati wa Yanga, Nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro', Kevin Yondan, Pato Ngonyani na Mtogo Vincent Bossou.
    Kakolanya pia amesaini Mkataba wa miaka miwili kujiunga na wafalme hao wa soka ya Tanzania, Yanga SC, jambo ambalo ni pigo kwa mahasimu, Simba SC waliokuwa wanamtaka kipa huyo. 
    Kakolanya anakwenda kuungana na makipa watatu waliopo Yanga, Deo Munishi ‘Dida’, Ally Mustafa ‘Barthez’ na Benedicto Tinocco kufanya idadi ya makipa wanne.
    Hata hivyo, mustakabali wa Tinocco haueleweki sasa baada ya kusajiliwa kwa Kakolanya mwenye umri wa miaka 22, ambaye Prisons ilimuibua Mbaspo Academy.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DANTE LA MTIBWA SUGAR LADONDOKA JANGWANI MIAKA MIWILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top