• HABARI MPYA

    Saturday, November 03, 2012

    KINDA LA RUVU LACHUANA NA MAPRO WA AZAM, SIMBA YANGA KWA UFUNGAJI

    Kavumbangu wa Yanga

    Na Mahmoud Zubeiry
    CHIPUKIZI Seif Rashid wa Ruvu Shooting anakabana koo na wachezaji wa kigeni wa klabu tatu bora nchini katika kuwania ufungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam, Simba na Yanga.
    Seif amefunga mabao matano na kati ya hayo, manne amefunga dhidi ya tatu bora hao wa Ligi Kuu, Yanga mawili, Simba na Azam moja kila timu na analingana na ‘mapro’ Kipre Tcheche wa Azam, Felix Sunzu wa Simba na Didier Kavumbangu wa Yanga.
    Wengine wenye mabao matano ni Amir Omary wa JKT Oljoro ya Arusha na Amri Kiemba      wa Simba SC, wakati Hood Mayanja wa African Lyon FC ana mabao manne sawa na Peter Michael wa Prisons FC,  Emmanuel Okwi wa Simba SC na Daniel Lyangawa Coastal Union.
    Wengine wanaofukuzia tuzo hiyo, inayoshikiliwa na John Raphael Bocco wa Azam ni Hussein Javu wa Mtibwa Sugar FC, Paul Ndauka wa Ruvu Shooting, Paul Nonga     wa JKT Oljoro FC, Salum Kanoni wa Kagera Sugar, Nsa Job wa Coastal Union, Bocco  mwenyewe ‘Adebayor’ na Mbuyu Twite wa Yanga, ambao wote kila mmoja ana mabao matatu.
    Wanaofuatia ni Jerry Santo wa Coastal Union, Abdulhalim Humud wa Azam FC, Nadir Haroub   ‘Cannavaro’, Nizar Khalfan wa Yanga, Hassan Dilunga wa Ruvu Shooting, Seleman Kibuta wa Toto Africans, Mrisho Ngassa wa Simba SC, Themi Felix wa Kagera Sugar SC, Issa Kanduru wa Mgambo Shooting, Jerry Tegete, Simon Msuva wa Yanga, Jamal Mnyate wa Mtibwa Sugar na Said Swedi wa Coastal Union, ambao kila mmoja ana mabao mawili.
    Waliofanikiwa kutikisa nyavu mara moja kila mmoja hadi sasa ni Nassoro Masoud ‘Chollo’, Daniel Akuffo, Haruna Moshi ‘Boban’      wa Simba SC, Dickson Daudi wa Mtibwa Sugar, Edward Christopher  wa Simba SC, Freddy Chudu wa Prisons, Nassoro Gumbo wa Mgambo Shooting FC, Said Ahmad, Omary Changa, Credo Mwaipopo wa JKT Ruvu, Mohamed Netto, Robert Magadula wa Toto Africans, Amandus Nesta wa Kagera Sugar, Kipre Bolou wa Azam FC, Elias Maguri wa Prisons, Mohamed Hussein wa Toto Africans, Benedictor Mwamlangala wa Prisons na Ibrahim Hassan wa JKT Oljoro.
    Wengine ni Chande Magoja wa Mgambo Shooting, Shija Mkinna wa Kagera Sugar, Haruna Adolf     wa JKT Ruvu SC, Awadh Juma wa Mtibwa Sugar, Meshack David wa JKT Oljoro, Shaaban Nditi wa Mtibwa Sugar, Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting, Suleiman Kassim ‘Selembe’ wa Coastal Union, Paul Nyangwe wa Polisi Morogoro, John Matei wa Prisons, Hussein Swedi wa Ruvu Shooting, Salum Kipanga wa Mgambo Shooting, Severine Constantine wa Toto Africans na Amos Mgisa wa JKT Ruvu FC.
    Wengine ni Rafael Keyala wa Ruvu Shooting SC, Mussa Ngunda wa Mgambo Shooting, Jimmy Shoji, Jacob Mambia wa JKT Ruvu, Fully Maganga wa Mgambo, Juma Jabu wa Coastal Union, Salum Swedi wa Mtibwa Sugar FC, Lameck Dayton wa Coastal Union, Ally Khan wa JKT Ruvu, Hamisi Kiiza wa Yanga, Wilfred Ammeh wa Kagera Sugar, Malimi Busungu wa Polisi Morogoro, Said Suzan, Said Dilunga wa Ruvu Shooting, Mohamed Samatta wa African Lyon FC, Malegesi Mwangwa wa Kagera Sugar, Said Bahanuzi wa Yanga, Mokili Rambo wa Polisi Morogoro na Mohamed Mkopi wa Mtibwa Sugar.
    Wachezaji ambao wamejifunga mabao hadi sasa katika Ligi Kuu ni Cannavaro wa Yanga dhidi ya Toto mjini Mwanza, Jerry Santo wa Coastal dhidi ya Azam Cghamazi na Hassan Ramadhan wa Mtibwa dhidi ya Toto African.

    Felix Sunzu wa Simba kushoto akitibiwa na Dk Cossmass Kapinga katika moja ya mechi za timu hiyo
    WANAOWANIA KIATU CHA DHAHABU LIGI KUU:
    MCHEZAJI                 MABAO            TIMU
    Amir Omary                5                      JKT Oljoro FC
    Kipre Tchetche           5                      Azam FC
    Seif Rashid u20          5                      Ruvu Shooting SC
    Didier Kavumbagu      5                      Young Africans SC
    Felix Sunzu                5                      Simba SC
    Amri Kiemba               5                      Simba SC
    Hood Mayanja            4                      African Lyon FC
    Peter Michael             4                      Tanzania Prisons FC
    Emmanuel Okwi         4                      Simba SC
    Daniel Lyanga            4                      Coastal union SC
    Hussein Javu              3                      Mtibwa Sugar FC
    Paul Ndauka              3                      Ruvu Shooting SC
    Paul Nonga                3                      JKT Oljoro FC
    Salum Kanoni             3                      Kagera Sugar SC
    Nsa Job                      3                      Coastal union SC
    John Bocco                 3                      Azam FC
    Mbuyu Twite               3                      Young Africans SC
    Kipre Tcheche wa Azam

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: KINDA LA RUVU LACHUANA NA MAPRO WA AZAM, SIMBA YANGA KWA UFUNGAJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top