Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya ujio wa Balozi wa
kampuni ya Hennessy, bwana Cyrille Auriol, maandalizi ya mapokezi yake
yamepamba moto. Balozi Auriol atatua Dar es Salaam jumatatu akitokea Paris kwa
ziara ya siku tatu kabla ya kuelekea Nairobi kwa muendelezo wa ziara yake nchi
za Afrika Mashariki.
Akiwa Dar es Salaam Balozi Auriol atahudhuria matukio
mbalimbali
maalum ya chakula cha jioni na uonjaji wa kinywaji hicho
ambazo
zimeandaliwa ili kuwazawadia watumiaji wa kinywaji
hicho nchini ambao sasa wanafurahia kampeni ya kinywaji hicho iitwayo ‘ Flaunt
Your Taste’. |