• HABARI MPYA

    Saturday, August 18, 2012

    THEO WALCOTT NAYE SASA 'AWARUSHA ROHO' ARSENAL


    Now Arsene faces Walcott nightmare

    Theo Walcott
    ANAONDOKA? Theo Walcott, naye aanza kuwarusha roho Arsenal
    THEO WALCOTT bado hajasaini mkataba mpya Arsenal. Na kuna wasiwasi kwamba winga huyo wa kimataifa wa England atakuwa mchezaji mwingine mwenye jina kubwa kuondoka Emirates baada ya Robin van Persie kutimkia Manchester United.
    Kocha wa Arsenal, Wenger amesema: “Bado tunajaribu kuuongeza mkataba wake.”
    Wenger amempoteza Manahodha wake, Van Persie na Cesc Fabregas katika miezi 12 iliyopita, wakati kiungo Alex Song yupo karibu kuhamia Barcelona kwa ada ya pauni Milioni 15.
    Walcott, aliyezaliwa miaka 23 iliyopita, amebakiza mwaka mmoja tu katika mkataba wake na Wenger amesema: “Wakati mchezaji hataki kubaki, unamlazimisha au unamuacha aondoke.”

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: THEO WALCOTT NAYE SASA 'AWARUSHA ROHO' ARSENAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top