• HABARI MPYA

    Monday, August 20, 2012

    AIRTEL RISING STAR YAANZA LEO LIVE SUPER SPORT 9


    Na Princess Asia
    MICHUANO ya Airtel Rising Star, inayohusisha vijana walio na umri chini ya miaka 17, inaanza leo mjini Najirobi, Kenya na itakuwa ikirushwa live na Super Sport 9.
    Kikosi cha wachezaji 16 watakaoiwakilisha Tanzania kwenye mashindano hayo ya kimataifa itakayofikia tamati Agosti 25, mwaka huu tayari kipo Nairobi kupeperusha bendera nzuri yenye za kijani, bluu, nyeusi na njano.
    Kikosi hicho kinaundwa na Denis Richard, Juma Hamza, Abdul Selemani, Ishaka Shekolowa, Bakari Ally, Abdulatif Mohamed, George Joseph, Badilu Said, Said Kassim, Amos Ikungula, Paul Balama, Goodluck Mabiku, Joel Kasimula, Ibrahim Mtenga, Sntkony Angelo na Suleiman Yunus.
    Mashindano hayo yanayotarajiwa kuwa na ushindani mkali yatashirikisha wachezaji wengine nyota wa ARS kutoka nchi za Kenya, Uganda, Malawi, DRC, Congo Brazzaville, Nigeria, Ghana, Zambia, Niger, Gabon, Burkina Fasso, Sierra Leone, Chad, Madagascar mbali na Tanzania.
    Michuano hiyo itafuatiwa na kliniki ya soka ya kimataifa ambayo pia itafanyika Nairobi chini ya walimu wa soka la vijana kutoka klabu maarufu duniani ya Manchester United ya England. Kliniki kama hii ilifanyika mwaka jana kwenye uwanja wa kisasa wa soka mjini Dar es Salaam na kushirikisha vijana kutoka Kenya, Malawi, Sierra Leone na wenyeji Tanzania.
    Katika kliniki ya mwaka huu, Tanzania itawakilishwa na wachezaji sita miongoni mwao ni wavulana watatu na wasichana watatu ambao walioibuka kuwa wachezaji bora wakati wa fainali za Taifa jijini Dar es Salaam mwezi Juni.
    Airtel Rising Stars ni mpango kabambe wa kuibua na kukuza vipaji vya wanasoka wanaochipukia barani Afrika. Walengwa ni wavulana na wasichana wenye umri chini ya miaka kumi na saba ambao watapata fursa ya pekee ya kuonyesha vipaji vyao mbele ya waatalum wa mpira wa miguu wa kitaifa na kimataifa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AIRTEL RISING STAR YAANZA LEO LIVE SUPER SPORT 9 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top