• HABARI MPYA

  Friday, August 05, 2016

  SIMBA SC WAREJEA DAR, WAINGIA KAMBINI NDEGE BEACH

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC imehamisha kambi yake kutoka Morogoro hadi Dar es Salaam leo.
  Simba SC imeingia kambini Dege Beach Hotel, Dar es Salaam leo ikitokea Chuo cha Biblia mjini Morogoro.  
  Kikosi kimelazimika kuwahi Dar es Salaam kwa ajili ya kuazimisha wiki ya Simba kuelekea kielele cha sherehe za miaka 80 ya klabu, maarufu kama Simba Day Jumatatu ijayo.
  Na Simba SC imekuja mjini siku moja baada ya kufungwa 1-0 na KMC ya Kinondoni jioni ya Jumatano katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Highlands, Bigwa mkoani Morogoro.
  Kikosi cha Simba kilichofungwa 1-0 na KMC jana

  Huo ulikuwa mchezo wa kwanza Simba SC kupoteza chini ya kocha mpya, Mcameroon, Joseph Marius Omog baada ya awali kushinda mechi zote tatu, 5-0 dhidi ya Burkina Fasso, 2-0 dhidi ya Moro Kids na 6-0 dhidi ya Polisi Morogoro.
  Katika kilele cha sherehe za Simba Day, Wekundu wa hao Msimbazi watamenyana na AFC Leopards ya Kenya iliyochukua nafasi ya Interclube ya Angola ambayo imejitoa dakika za mwishoni.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC WAREJEA DAR, WAINGIA KAMBINI NDEGE BEACH Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top