• HABARI MPYA

  Monday, June 20, 2016

  YANGA YAPAMBANA, YAPIGWA 1-0 KWA MBINDE BEJAIA

  Na Mwandishi Wetu, BEJAIA
  YANGA SC imeanza vibaya mechi za Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika, baada ya kufungwa bao 1-0 wenyeji Mouloudia Olympique Bejaia Uwanja wa Unite Maghrebine mjini Bejaia usiku huu.
  Yanga ilimaliza pungufu mchezo huo baada ya beki wake wa kushoto, Mwinyi Hajji Mngwali kuonyeshwa kwa kadi ya pili ya njano na kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 90. 
  Na Mwinyi alitolewa baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Oscar Joshua kipindi cha kwanza.
  Shujaa wa MO Bejaia alikuwa ni beki Yassine Salhi aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 20, akimalizia kazi nzuri ya mshambuliaji Ismail Belkacemi. 
  Matokeo hayo yanaifanya MO Bejaia ishike nafasi ya pili katika kundi hilo, nyuma ya TP Mazembe ambayo iliifunga Medeama ya Ghana 3-1 katika mchezo wa kwanza mjiji Lubumbashi Jumapili, wakati Yanga inashika nafasi ya tatu.
  Mechi zijazo za kundi hilo, Yanga watakuwa wenyeji wa Mazembe Dar es Salaam na Medeama wataikaribisha Mo Bejaia. 
  Kikosi kamili cha Yanga kinachoanza ni; Deogratius Munishi 'Dida', Mbuyu Twite, Oscar Joshua/Mwinyi Hajji dk33, Kelvin  Yondani, Vicent Bossou, Thabani Kamusoko, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Donald Ngoma, Amissi Tambwe/Matheo Anthony dk85 na Deus Kaseke/Geoffrey Mwashiuya dk75.
  MO Bejaia; C. Rahmani, A. Messaoudi, A. Lakhdari, S. Baouali, S. Khadir, Y. Salhi/ M. Betorangal dk71, S. Benali, S. Sidibé, M. Ferhat/A. Mouhli dk87, M. Athmani na I. Belkacemi/ B. Bendjelloul dk79.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAPAMBANA, YAPIGWA 1-0 KWA MBINDE BEJAIA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top