• HABARI MPYA

  Saturday, June 18, 2016

  WANYAMA AENDA KUKAMILISHA UHAMISHO WAKE SPURS

  KIUNGO Mkenya wa Southampton, Victor Wanyama (pichani kushoto) anatarajia kuaini Mkataba wa kuhamia Tottenham Hotspur.
  Spurs imewapiku mabingwa watetezi, Leicester City katika kuwania saini ya Wanyama, kiungo mkabaji mwenye thamani ya juu na atasaini Jumatatu wiki ijayo.
  Wanyama alikuwa gereza la Kamiti Maximum mjini Nairobi Jumamosi ambako pia alizungumzia uhamisho wake.
  "Nataka kuwashukuru Southampton kwa nafasi kubwa waliyonipa kucheza England. Kama mwanasoka, kuhamia kwangu Tottenham Hotspur kutanipa nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa," alisema.
  Spurs ilijaribu kumsaini mchezaji huyo mwanzoni mwa msimu, lakini Southampton ikagoma kumuuuza Wanyama na akacheza mechi 35 zaidi.
  Wanyama ataondoka Nairobi Jumapili kwenda London ambako anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake Jumatatu na kuungana tena na kocha Mauricio Pochettino ambaye alimsajili The Saints miaka mitatu iliyopita.
  Hiyo itakuwa klabu ya Uingereza kwa Wanyama aliyejiunga na Southampton kutoka Celtic ambako kipaji chake kilimvutia Pochettino.
  Safari yake ya Ulaya ilianzia kwa klabu ya Germinal Beerschot ya Ubelgiji kabla ya kuhamia kwa vigogo wa Scotland, ambako ndiko alikopatia umaarufu wake baada ya kufunga bao la ushindi akicheza Ligi ya Mabingwa dhidi ya Barcelona. Anatarajiwa kurejea Nairobi Jumatano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WANYAMA AENDA KUKAMILISHA UHAMISHO WAKE SPURS Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top