• HABARI MPYA

  Tuesday, June 21, 2016

  WAGENI 'WAWAZIMISHA' WENYEJI NYUMBANI LIGI YA MABINGWA

  USHINDI wa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na Zamalek ya Misri Jumapili ulifanya timu hizo zianze vyema ugenini katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwishoni mwa wiki.
  Baada ya wenyeji Zesco United ya Zambia kushinda mechi yao ya kwanza Jumamosi, Wydad Casablanca ya Morocco ikaendeleza wimbi la timu kuvuna pointi ugenini kwenye michuano hiyo.
  Mabao ya Tiyani Mabunda na Khama Billiat yaliipa Sundowns ushindi wa 2-0 dhidi ya mabingwa mara mbili Afrika, Entente Setif ya Algeria katika mchezo wa Kundi B ambao ulitawaliwa na vurugu za mashabiki. 

  Mashabiki wa nyumbani waliopagawa na kipigo walirusha chupa za plastiki uwanjani.
  Sundowns, iliyotolewa katika hatua ya mwisho ya kufuzu kwenye makundi kabla ya kurejeshwa baada ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuondolewa mashindanoni, ilifunga mabao mawili babu kubwa. 
  Bao pekee la mapema la Bassem Morsy likaipa ushindi wa 1-0 Zamalek nchini Nigeria dhidi ya Enyimba mjini Port Harcout, ambayo imefunga mabao 10 katika mechi tatu za nyumbani wakati wa hatua za kufuzu. 
  Zesco iliwaduwaza mabingwa wa kihistoria wa Afrika, Al Ahly ya Misri kwa kuwafunga 3-2 na Wydad ikashinda 1-0 dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast katika mchezo mwingine. Mechi za pili zinatarajiwa kuchezwa kati ya Juni 28 na 29.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAGENI 'WAWAZIMISHA' WENYEJI NYUMBANI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top