• HABARI MPYA

  Tuesday, June 14, 2016

  TELELA AAMUA KUREJEA DARASANI BAADA YA KUTEMWA YANGA

  Na Saada Mohammed, DAR ES SALAAM
  KIUNGO mjuvi kweli wa soka, Salum Abdul Telela ‘Master’ (pichani kulia) amesema kwamba anarejea shule kusoma baada ya klabu yake, Yanga SC kukataa kumuongezea Mkataba na lengo ni kuwa msomi wa kiwango cha juu baada ya miaka michache. 
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE leo, Telela amesema kwamba anakwenda kufanya Stashahada kwanza, baadaye ataunganisha Shahada na baada ya hapo ataendelea na safari yake ya kielimu. 
  “Kwa sasa ninarejea darasani tu, ninarudi kusoma ili kujiandaa kwa maisha mengine, napumzika kidogo mpira,”amesema.
  Alipoulizwa iwapo itatokea timu ya kutaka kumsajili kwa ofa nzuri, anaweza kubadili msimamo wake, Telelea alisema; “Kwa sasa nafikiria kurudi shule tu kwanza,”. 
  Hatua hiyo inafutia Telela kutoongezewa Mkataba, licha ya umuhimu wake wa wazi unaoonekana katika timu kwa sababu ni kiraka anayeweza kucheza kama beki wa kulia, kati na nafasi zote za kiungo.
  Na kuhusu suala la nidhamu, Telela anaonekana ni mchezaji mwenye nidhamu, bidii ya mazoezi na kujituma, ambaye wakati wote anapoingizwa uwanjani licha ya muda mwingi kuwa mchezaji wa akiba hucheza vizuri. 
  Wachezaji wa Yanga wamesikitishwa na uamuzi wa kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm kumtema Telela, kwani licha ya ufundi wake kisoka, pia alikuwa rafiki wa kila mtu katika timu.
  Na hata baadhi ya viongozi wa Yanga bado wanapingana na uamuzi wa Pluijm kumtema Telela ambaye amdumu Yanga tangu mwaka 2011 aliposajiliwa mara ya kwanza kutoka Moro United.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TELELA AAMUA KUREJEA DARASANI BAADA YA KUTEMWA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top