• HABARI MPYA

  Monday, June 06, 2016

  MALINZI KUKUTANA NA YANGA KUMALIZA TOFAUTI ZA UCHAGUZI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kesho asubuhi anatarajiwa kukutana na uongozi wa Yanga kujadili naye juu ya mvutano ulioibuka kuhusu uchaguzi wa klabu hiyo.
  Malinzi amesema katika kikao hicho Sekretarieti ya TFF pia kujadili na kupanga namna ya kufikia suluhisho la migongano iliyotokea.
  Mvutano umeibuka kuhusu uchaguzi wa Yanga SC ambao sasa unawaacha njia panda wanachama wa klabu hiyo, wakiwa hawajui washike lipi.
  Hiyo inafuatia TFF kutangaza na kuendesha mchakato wa uchaguzi wa klabu hiyo - wakati huo huo Yanga nayo ikitangaza na kuendesha mchakato wake huo yenyewe.
  Rais wa TFF, Jamal Malinzi ameingilia rasmi mgogoro wa uchaguzi wa Yanga
  Yanga imesema uchaguzi wake utafanyika Juni 11 na na TFF imesema utafanyika Juni 25. Na wote, TFF na Yanga wamenza kutoa fomu za kugombea wiki iliyopita. 
  Waliochukua fomu TFF ni Aaron Nyanda, Titus Osoro wanaowania nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Paschal Laizer, Edgar Chibula, Mohammed Mattaka, Mchafu Ahmed Chakoma, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’ Omari Said kutoka Zanzibar wanaowania Ujumbe wa Kamati ya Utendaji, wakati miongoni mwa waliochukua fomu Yanga ni pamoja na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Ayoub Nyenzi.
  Wakati mvutano huo, ukiendelea uongozi wa Yanga ukaibua tuhuma za TFF kwa kushirikiana na Kamati yake ya Uchaguzi chini ya Mwenyekiti, Wakili Alloyce Komba kupanga njama za kumkata Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yussuf Manji.
  Kwa tuhuma hizo, mwishoni mwa wiki Wakili Komba alitangaza kujitoa kusimamia mchakato wa uchaguzi wa Yanga. Leo Yanga imefikisha tuhuma hizo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MALINZI KUKUTANA NA YANGA KUMALIZA TOFAUTI ZA UCHAGUZI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top