• HABARI MPYA

    Monday, June 06, 2016

    ‘ALIYEIPA’ YANGA MATAJI MATATU AINGIZWA KAMATI YA MASHINDANO YA TFF

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MWENYEKITI wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Isaac Chanji ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
    Uteuzi huo umefanyika katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya TFF, chini ya Rais wake, Jamal Malinzi kilichofanyika Jumapili mjini Dar es Salaam. 
    Bila shaka uteuzi wa Chanji umezingatia mafanikio yake Yanga akiiwezesha klabu kutwaa mataji yote matatu nchini, Ngao ya Jamii, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Kombe la TFF, maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).
    Yanga pia imefuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika mwaka huu – zote zikihesabiwa kama kazi nzuri za Chanji. 
    Mwenyekiti wa kamati ya Mashindano ya Yanga, Isaac Chanji (kulia) akizungumza na mshambuliaji wa timu yake, Mzimbabwe, Donald Ngoma 

    Katika Kamati hiyo, Chanji atakuwa chini ya Mwenyekiti, Geofrey Nyange ‘Kaburu’, ambaye pia ni Makamu Rais wa Simba SC, Makamu Mwenyekiti, Ramadhan Nassib na Wajumeb wengine James Mhagama na Clemence Sanga, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Yanga.
    Kamati Ya Nidhamu itaendelea kuwa chini ya Mwenyekiti, Tarimba Abbas, Makamu wake Wakili Jerome Msemwa na Wajumbe Kassim Dau, Nassoro Duduma na Kitwana Manara.
    Kamati Ya Rufani Ya Nidhamu sasa itakuwa chini ya Wakili Alloyce Komba, Makamu wake wakili Abdallah Gonzi na Wajumbe Abdalla Mkumbura, Dk Francis Michael na Wakili Twaha Mtengela.
    Kamati Ya Maadili itakuwa chini ya Wakili Wilson Ogunde Mwenyekiti, Makamu wake Ebeanazer Mshana na Wajumbe Mhandisi, Mahende Mgaya na Wabunge Said Mtanda na Glorius Luoga.
    Kamati ya Rufaa ya Maadili Mwenyekiti wake Wakili Walter Chipeta, Makamu wake Jaji George Gisangeta na Wajumbe , Lilian Kitomari Mbunge Faustine Ndugulile na Bakili Bakari Anga.
    Kamati ya Uchaguzi sasa itakuwa chini ya Mwenyekiti Wakili Revocatus Kuuli, Makamju wake Domina Madeli na Wajumbe Hamidu Mahmoud Omar, Jeremiah John Wambura na Juma Lalika.
    Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi itaendelea kuwa chini ya Mwenyekiti Wakili Julius Lugaziya, Wakili Macher Suguta na Wajumbe Juma Abeid Khamis, Rashid Dilunga na Joseph Mapunda.
    Kamati ya Katiba Sheria na Hadhi za Wachezji 
    itaendelea kuwa chini ya Mwenyekiti Richard Sinamtwa, Makamu wake Wakili Raymond Wawa na Wajumbe Pascal Kihanga, Benister Lugora na David Machumu.
    Kamati ya Fedha na Mipango itaendelea kuwa chini ya Mwenyekiti Wallace Karia, ambaye pia ni Makamu wa Rais wa TFF, Makamu wake, Omari Walii na Wajumbe Goodluck Moshi, Ellie Mbise na Deo Lubuva.
    Kamati ya Ufundi itaendelea kuwa chini ya Mwenyekiti Kidao Wilfred, Makamu wake Vedastus Rufano na Wajumbe Ahmed Mgoyi, Dan Korosso na Pelegrinius Rutahyugwa.
    Kamati ya Soka Vijana itaendelea kuwa chini ya Mwenyekiti, Ayoub Nyenzi, Makamu wake Khalid Abdallah na Wajumbe Steven Njowoka, Mulamu Ngh’ambi na Stewert Massima.
    Kamati ya Soka ya Wanawake itaendelea kuwa chini ya Mwenyekiti Amina Karuma, Makamu wake, Rose Kisiwa na Wajumbe Zena Chande, Zafarani Damoder, Beatrice Mgaya, Sofia Tigalyoma na Ingridy Kimario.
    Kamati ya Waamuzi itakuwa chini ya Mwenyekiti Saloum Umande, Makamu wake, Nassoro Said na Wajumbe Charles Ndagala, Kanali Issaro Chacha, Soud Abdi na Ofisa wa dawati la marefa wa TFF.
    Kamati ta Habari na Masoko itakuwa chini ya Mwenyekiti Athumani Kambi, Makamu wake Blassy Kiondo na Wajumbe, Grace Hoka, Amir Mhando na Haroub Selemani.
    Kamati ya Ukaguzi Wa Fedha itakuwa chini ya Mwenyekiti Yahya Hamad, Makamu wake Mkaguzi Abdallah Mussa na Wajumbe Jackson Songoro, Golden Sanga na Cyprian Kwiyava.
    Kamati ya Tiba itakuwa chini ya Mwenyekiti Dk Paul Marealle, Makamu wake Fred Limbanga na Wajumbe Dk Mwanandi Mwankemwa, Dk Eliezer Mdelema na Dk Asha Mecky Sadik.
    Kamati ya Futsal na Soka ya Ufukweni itakuwa chini ya Mwenyekiti Ahmed Idd Mgoyi, Makamu wake, Hussein Mwamba na Wajumbe 
    Samson Kaliro, Boniface Pawassa na Apollo Kiyungi.
    Mfuko wa Maendeleo ya Soka utakuwa chini ya Mwenyekiti, Tido Mhando na Wajumbe Beatrice Singano, Salum Rupia, Ephraim Mafuru, Tarimba Abbas, Meshack Bandawe na Joseph Kahama.
    Kamati ya Ajira itakuwa chini ya Mwenyekiti  Wallace Karia, Makamu wake Vedastus Rufano na Wajumbe Selestine Mwesigwa, Said Mohamed na Salum Umande Chama.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ‘ALIYEIPA’ YANGA MATAJI MATATU AINGIZWA KAMATI YA MASHINDANO YA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top