• HABARI MPYA

    Monday, July 17, 2017

    MAJJID AREJESHWA KWENYE UONGOZI YANGA

    Na Shekha Jamal, DAR ES SALAAM
    MWANACHAMA maarufu wa Yanga, Majjid Suleiman amerejeshwa kwenye uongozi wa klabu baada ya muda mrefu, kufuatia kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji.
    Uteuzi huo umefanywa juzi katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya klabu, chini ya Kaimu Mwenyekiti, Clement Sanga.
    Taarifa ya Yanga kwa vyombo vya Habari leo imesema kwamba kwa mujibu wa Katiba ya klabu, Kaimu Mwenyekiti ameteua Wajumbe watatu kujaza nafasi zilizoachwa wazi na Wajumbe waliojiuzulu, akiwemo Mhandisi Paul Malume.
    Malume aliyekuwa pia Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga baada ya kuondoka kwa Isaac Chanji – naye  amelazimika kuachia nafasi hizo ili kwenda masomoni nje ya nchi.
    Majjid Suleiman (kushoto) alipokuwa kwenye Kamati ya Mashindano pamoja na Abdallah Bin Kleb (katikati) walifanikiwa kumleta kocha Mholanzi, Ernie Brandts  
    Mbali na Majjid, kiongozi wa Yanga tangu miaka ya 1990 enzi hizo akiwa mtu wa karibu wa mfadhili wa zamani wa klabu, Abbas Gulamali (sasa) marehemu, Wajumbe wengine walioteuliwani Mohammed Nyenge na Tonny Mark.
    Katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya Yanga juzi, uongozi umekubaliana kuwashirikisha wachezaji wa zamani katika masuala ya klabu na kuwaweka karibu na timu, kujenga umoja wao wana Yanga kwa ujumla na kuunda safu ya uongozi wao itakayorahisisha mawasiliano baina yao na uongozi wa klabu.
    Imekubaliwa pia kuweka kumbukumbu kwa ajili ya historia ya klabu na vizazi vijavyo kupitia wachezaji wa zamani na kusaidiana katika suala zima la ugunduzi wa vipaji vya wachezaji kwa manufaa ya klabu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAJJID AREJESHWA KWENYE UONGOZI YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top