Kevin Yondan |
Na Prince Akbar
BEKI wa
Yanga, Kevin Yondan amesema kwamba licha ua kuwafunga Kenya, Harambee Stars,
lakini wapinzani wao hao ni wazuri na zaidi akamsifia mshambuliaji wa klabu ya Daraja
la Pili Ufaransa, AJ Auxerre, Dennies Oliech kwamba ni mtu hatari.
Akizungumza
na BIN
ZUBEIRY kwa simu kutoka Mwanza jana, Yondan alisema kwamba walifanya
kazi kubwa mno kumdhibiti Oliech, kwani mtu huyo ni hatari.
“Yule jamaa
anajua, mimi binafsi ilinibidi nitulize sana akili katika kukabiliana naye,
ndiyo maana hakufunga, bila hivyo Yule mtu angefunga,”alisema Yondan.
Hata hivyo,
beki huyo wa kati alisema timu yao ilicheza vizuri kwa ujumla jana na anaamini
hizi ni dalili nzuri za kuwapa Watanzania.
“Tunamshukuru
Mungu kwa ushindi huu, lakini tunaendelea kuomba mashabiki wetu waendelee
kutupa sapoti ili tufanye vizuri zaidi,”alisema.
Taifa Stars,
jana iliibwaga Kenya, Harambee Stars bao 1-0 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini
Mwanza katika mchezo wa kirafiki ulio katika kalenda ya Shirikisho la Soka la
Kimataifa (FIFA).
Hadi
mapumziko, Stars ilikuwa mbele kwa bao 1-0, lililotiwa kimiani na beki Aggrey
Morris katika dakika ya nne, baada ya kupanda kusaidia mashambulizi.
Katika mechi
hiyo iliyochezeshwa na refa anayetambuliwa na FIFA, Oden Mbaga, Kenya
walitawala dakika 10 za mwanzo, lakini baada ya hapo Stars wakafunguka nao na
kuanza kula nao sahani moja na Harambee Stars.
Kipindi cha
pili, Kenya walianza na mabadiliko kocha Henri Michel akiwapumzisha James
Situma, Jerry Santo na Wesley Kemboi na kuwaingiza Christopher Wekesa, Anthony
Akumu na Timbe Ayoub.
Pamoja na
mabadiliko hayo, mambo yaliendelea kuwa magumu kwa Harambee Stars, kwani
wenyeji waliendelea kucheza kwa makini, wakishambulia na kujilinda zaidi.
Kocha wa
Stars naye, Mdemnark, Kim Poulsen aliwatoa Amir Maftah, Salum Abubakar, Mwinyi
Kazimoto, Mbwana Samatta, Mrisho Ngassa na Thomas Ulimwengu na kuwaingiza
Nassor Masoud ‘Chollo’, Amri Kiemba, Simon Msuva, John Bocco ‘Adebayor’,
Shaaban Nditi na Issa Rashid.
Baada ya
mchezo huo, kocha wa Harambee, Mfaransa Michel alionyesha kukerwa na matokeo
hayo na kusema timu yake haikucheza vizuri, wakati Polusen, amefurahia ushindi
huo akisema timu yake haijacheza kwa miezi miwili na baada ya siku mbili za
mazoezi wameifunga Kenya.
Taifa Stars; Juma Kaseja, Shomari Kapombe, Amir
Maftah/Nassor Masoud ‘Chollo’ dk70, Aggrey Morris, Kevin Yondan, Frank Domayo,
Salum Abubakar/Amri Kiemba dk69, Mwinyi Kazimoto/Simon Msuva dk69, Mbwana
Samatta/John Bocco dk 84, Mrisho Ngassa/Shaaban Nditi dk72 na Thomas Ulimwengu/Issa
Rashid dk 89.
Harambee Stars; Frederick Onyango, Brian Mandela,
Eugene Asike, James Situma/Christopher Wekesa dk 46, Edwin Wafula, Jerry
Santo/Anthony Akumu dk 46, Peter Opiyo/Charles Okwemba dk 67, Patrick Obuya,
Patrick Osaika/Mulienge Ndeto dk 73, Dennis Oliech na Wesley Kemboi/Timbe Ayoub
dk 46.
REKODI YA STARS MWAKA HUU NA RATIBA
YA MECHI ZIJAZO:
Februari 23, 2012
Tanzania 0 – 0 DRC (Kirafiki)
Februari 29, 2012
Tanzania 1 – 1 Msumbiji (Kufuzu Mataifa ya Afrika)
Mei 26, 2012
Tanzania 0 – 0 Malawi
Juni 2, 2012
Ivory Coast
2 – 0 Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)
Juni 10, 2012
Tanzania 2 – 1 Gambia (Kufuzu Kombe la Dunia)
Juni 17, 2012
Msumbiji 1 –
1 Tanzania (Tanzania ilitolewa kwa
penalti kufuzu Mataifa ya Afrika)
Agosti 15, 2012
Botswana 3 –
3 Tanzania (Kirafiki)
Novemba 14, 2012
Tanzania 1-0 Kenya
(Kirafiki)
Machi 22, 2013
Tanzania Vs Morocco (Kufuzu Kombe la Dunia)
Juni 7, 2013
Morocco Vs Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)
Juni 14, 2013
Tanzania Vs Ivory Coast (Kufuzu
Kombe la Dunia)
Septemba 6, 2013
Gambia Vs Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)