• HABARI MPYA

    Wednesday, November 14, 2012

    TFF YAREKEBISHA VIINGILIO MECHI YA SERENGETI NA KONGO JUMAPILI


    Na Prince Akbar
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limefanya mabadiliko ya viingilio vya mechi ya raundi ya mwisho ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa vijana chini ya umri chini ya miaka 17 kati ya wenyeji, Serengeti Boys na Kongo Brazzaville itakayochezwa Jumapili wiki hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo amesema leo kwamba awali kiingilio cha juu katika mechi hiyo itakayoanza saa 10:00 jioni kilikuwa Sh. 5,000, lakini kwa lengo la kuwafanya wadau wa kiingilio hicho kuchangia gharama za mechi hiyo sasa kutakuwa na viingilio vitatu tofauti katika viti vya VIP.
    Wambura amesema VIP A ambayo ina viti 748 kiingilio kitakuwa sh. 10,000, VIP B inayochukua watazamaji 4,160 kiingilio ni sh. 5,000 wakati VIP C yenye viti 4,060 kiingilio ni sh. 2,000. Kwa sehemu nyingine (viti vya rangi ya chungwa, kijani na bluu) ambavyo jumla yake ni 48,590 kiingilio kitabaki kuwa sh. 1,000.
    Amesema Kongo Brazzaville inatarajia kuwasili leo kwa ndege ya Ethiopian Airlines na itafikia katika hoteli ya Sapphire Court, Kariakoo, Dar es Salaam.
    Wakati huo huo, Kamati ya kusaidia Serengeti Boys ishinde, chini ya Mwenyekiti wake, Ridhiwani Jakaya Kikwete, itakutana na Waandishi wa Habari kesho Saa 5:00 asubuhi katika hoteli ya JB Belmont, ukumbi wa Ngorongoro, Dar es Salaam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: TFF YAREKEBISHA VIINGILIO MECHI YA SERENGETI NA KONGO JUMAPILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top