Na Mahmoud Zubeiry
MASHINDANO
ya Riadha ya 11 ya Kilimanjaro Marathon yanatarajiwa kufanyika Machi 3, mwakani
mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza
kwenye uzinduzi wa mashindano hayo usiku huu katika hoteli ya JB Belmonte mjini
Dar es salaam, Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bi.
Kushilla Thomas alisema bia ya Kilimanjaro Premium Lager inaendelea na udhamini
wa mbio hizo zinazoendelea kuwa kubwa na bora kila mwaka huku zikiibua vipaji
vipya na kuwapa wanariadha chipukizi fursa ya kukua na kuweza kushindana
kimataifa.
“Kilimanjaro
Premium Lager inalenga kuendeleza riadha kwa kukuza vipaji, kuwapa wanariadha
wetu jukwaa la kushindania na wanariadha kutoka mataifa mbalimbali.” Alisema
Kushilla.
Aliongeza
kuwa bia ya Kilimanjaro Premium Lager ina lengo la kuhakikisha mashindano hayo
yanakuwa na mvuto kwa wanariadha wenye vipaji ili kuongeza ubora wa riadha ya
Tanzania ili Watanzania waweze kushiriki kikamilifu kwenye mashindano makubwa
duniani.
Kwa upande
wake, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema:
“Kupata washiriki kutoka nchi mbalimbali inatusaidia kuonyesha dunia kuwa
Kilimanjaro Marathon nini lakini kuwaendeleza na kuwapa moyo wanariadha Watanzania
ni kipaumbele chetu kikubwa, kwa sababu hiyo tumeanzisha zawadi maalum ya
shilingi milioni 3 kwa Watanzania watakaomaliza wakiwa wa kwanza katika mbio za
42km Kilimanjaro Premium Lager Marathon na hii ni mbali na zawadi watayopata
kwa nafasi watakazoshinda.”
“Maandalizi
ya Kilimanjaro Marathon 2013 yameishaanza ili kuhakikisha mbio hizo zinakuwa
bora kama ilivyo utamaduni wetu kuhakikisha tunaboresha kila mwaka ili kuwapa
raha ya aina yake washiriki pamoja na watazamaji.”
“Kwa mara nyingine tena, Kilimanjaro Premium
Lager itaendelea kuwathamini wanariadha kwa kuwatunuku zawadi nzuri ya fedha
taslimu huku ikiwapa watazamaji burudani ya aina yake.”
Zawadi ya
fedha taslimu kwa washindi wa kwanza hadi wa tatu wanaume kwa wanawake kwenye
mbio ndefu za km 42.195 zijulikanazo kama Kilimanjaro Premium Lager Marathon
itakuwa ni shilingi milioni 3 , washindi wa pili watajipatia shilingi milioni
1.5 kila mmoja huku washindi wa tatu wakijipatia shilingi 850,000 kila mmoja.
Zawadi nhii itakuwa ni kivutio kwa wanariadha mashuhuri kushiriki katika mbio
hizi zinazoingia mwaka wa 11 tangu kuanzishwa.
Utepe unakatwa |
Crew ya wadhamini wa Kili Marathon |
Kushilla akizungumza |
Kavishe akizungumza |
Kushoto ni Rais wa PARALIMPIKI, Johonson Jasson na kulia na Nyambui |
Kavishe akizungumza na John Addison, Mkurugenzi wa Wild Frontiers, waandaaji wa Kili Marathon |
Mkurugenzi wa Executive Solutions, Aggrey Marealle akizungumza |
Mohamed Omar wa KK Security |
Walimbwende wa Executive Solutions |