// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); BAHANUZI, CANNAVARO 'WATEREMSHWA' KWENYE NDEGE WAKIMFUATA DROGBA CHINA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BAHANUZI, CANNAVARO 'WATEREMSHWA' KWENYE NDEGE WAKIMFUATA DROGBA CHINA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, November 13, 2012

    BAHANUZI, CANNAVARO 'WATEREMSHWA' KWENYE NDEGE WAKIMFUATA DROGBA CHINA

    Bahanuzi

    Na Mahmoud Zubeiry
    WACHEZAJI wawili wa Yanga, beki Nadir Haroub Ally ‘Cannavaro’ na mshambuliaji Said Rashid Bahanuzi waliotarajiwa kuondoka leo saa 10:00 jioni kwa ndege ya Qatar Airways kwenda China, kufanya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa, wamezuiwa na klabua yao hiyo.
    Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Abdallah Ahmad Bin Kleb ameiambia BIN ZUBEIRY mida hii kwamba, sababu za kuzuiwa kwa wachezaji hao ni kutokana na klabu inayowataka kutofuata taratibu.
    “Hawajatuma barua, hawa wanataka kwenda kienyeji tu, na sisi si kama tumewazuia, tumeitaka kwanza hiyo klabu ifuate taratibu kwa kutuma barua huku na kujitambulisha, ili hata hao wachezaji wakipata matatizo tujue tunaanzia wapi,”alisema Bin aKleb.
    Mapema leo, Cannavaro, Nahodha Msaidizi wa Yanga aliiambia BIN ZUBEIRY kwamba wanakwenda China kwa wiki mbili na baada ya majaribio kama wakifuzu, klabu inayowataka itafanya mazungumzo na klabu yao.
    “Sisi wote tuna mikataba na klabu, hivyo tukifuzu jamaa itabidi watuhamishe Yanga,”alisema  beki huyo kati aliyezaliwa Februari 10, mwaka 1982.
    Cannavaro yupo Yanga tangu mwaka 2006, aliposajiliwa kutoka Malindi ya Zanzibar wakati Bahanuzi amesajiliwa msimu huu akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro.
    Mwaka 2009, Cannavaro alichukuliwa kwa mkopo na klabu ya Vancouver Whitecaps ya Canada na baada ya miezi sita alirejeshwa Yanga alikoendelea kucheza hadi leo anakwenda kujaribu bahati yake China.
    Bahanuzi ameingia na zali la aina yake Yanga SC, kwani katika mashindano ya kwanza kuichezea klabu hiyo alifanikiwa kuibuka mfungaji bora wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na kati, Kombe la Kagame.
    Hadi sasa, Said Bahanuzi   maarufu kama Spider Man, ameifungia Yanga mabao 12 katika mechi 14, yakiwemo matatau ya penalti tangu ajiunge na timu hiyo Julai mwaka huu.
    Kwa sasa China ni nchi ambayo mastaa wengi waliokuwa Ulaya wanakwenda kumalizia soka yao, mfano washambuliaji wawili wa zamani wa Cheslea, Didier Drogba na Nicolas Anelka waliopo Shenghua Shanghai. Anelka ni kocha mchezaji.    
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: BAHANUZI, CANNAVARO 'WATEREMSHWA' KWENYE NDEGE WAKIMFUATA DROGBA CHINA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top