BANDARI ya Mombasa,
Kenya inayopigwa tafu na wachezaji wanne wa Kitanzania, David Naftali (pichani), Meshack
Abel, Mohamed Banka na Thomas Maurice, imeendelea kujiimarisha katika harakati
za kurejea Ligi Kuu ya Kenya, baada ya leo kuifunga mabao 3-1 Iron Strikers.
Mabao ya Bandari ambayo
msimu huu imempoteza kipa Mtanzania, Ivo Mapunda aliyehamia Gor Mahia,
yalifungwa na Erick Okoth, kiungo wa zamani wa Azam FC, Crispin Odula na
mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Tomas Maurice, kwa mpira wa adhabu.
Maurice, ambaye pia
amewahi kuchezea Mtibwa Sugar, ndiye alikuwa nyota wa mchezo wa leo, kwa mujibu
wa beki wa Bandari, Naftali aliyewahi kuchezea Simba SC.
Ushindi huo, unaifanya
Bandari iliyoshuka Daraja msimu uliopita, kuendelea kuongoza Ligi Daraja la Kwanza
Kenya, baada ya kufikisha pointi 57, ikifuatiwa na Sharks Kariobang, yenye
pointi 48, ambayo leo imetoka sare na timu ya zamani ya mshambuliaji wa AJ
Auxerre ya Ufaransa, Dennis Oliech, Mathare United.
|
0 comments:
Post a Comment