• HABARI MPYA

  Friday, July 07, 2017

  HUZUNI, SHABIKI MDOGO WA SUNDERLAND, BRADLEY AFARIKI DUNIA

  SHABIKI maarufu mtoto mdogo wa klabu ya Sunderland ya England, Bradley Lowery amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka sita baada ya kusumbuliwa na maradhi ya saratani kwa muda mrefu.
  Bradley alikuwa anaugua ugonjwa ambao wa Kiingereza hufahamika kama Neuroblastoma - aina nadra ya saratani - tangu alipokuwa na umri wa miezi 18.
  Bradley alifanywa kuwa kibonzo-nembo wa klabu hiyo na akaunda urafiki wa karibu na mshambuliaji wa klabu hiyo Jermain Defoe.

  Mtoto wa miaka sita, Bradley Lowery (pichani na mama yake, Gemma) amefariki dunia leo katika mikono ya mama yake baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani kwa muda mrefu PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  Aidha, aliongoza wachezaji wa England kuingia uwanjani Wembley wakati wa mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Lithuania.
  Kifo chake kimethibitishwa na wazazi wake kwenye mitandao ya kijamii.
  "Kijana wetu mkakamavu ameenda kuwa na malaika leo.
  "Alikuwa shujaa wetu na alipigana sana lakini alihitajika kwingine. Hatuna maneno ya kueleza jinsi tulivyohuzunishwa na kifo chake."
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HUZUNI, SHABIKI MDOGO WA SUNDERLAND, BRADLEY AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top