• HABARI MPYA

  Jumatano, Juni 28, 2017

  MORATA ASITISHA FUNGATE LAKE SABABU YA MAN UNITED

  MSHAMBULIAJI Alvaro Morata amekatisha fungate lake Ibiza ili akashughulikie uhamisho wake kwenda Manchester United kwa mujibu wa gazeti la AS la Hispania.
  AS limeripoti kwamba Real Madrid amesafiri kutoka Ibiza kwenda nyumbani kwake mjini Madrid, huku mazungumzo ya uhamisho baina ya klabu hizo mbili yakiendelea.
  Morata amezungumza mara kadhaa kwa simu na kocha wa United, Jose Mourinho na imeripotiwa yuko njiani kuhamia Ligi Kuu ya England.

  Wanandoa hao wamekatisha fungate lao ili kwenda kushughulikia uhamisho wa mume kuhamia Ligi Kuu ya England PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  Kocha wa United, Mourinho amekuwa shabiki wa Morata tangu anamfundisha katika kipindi chake cha kufanya kazi kwa miaka mitatu Bernabeu.
  Mashetani Wekundu 'walitupa ndoana' zao kwa Morata mwezi uliopita, lakini Madrid inataka ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 70 kumuuza mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania.
  Mourinho anasaka mshambuliaji mpya Man United kwa sababu Zlatan Ibrahimovic anatarajiwa kuondoka siku si nyingi zijazo. 
  Awali United walimtaka sana Antoine Griezmann, lakini Mfaransa huyo akaamua kusaini mkataba mpya Atletico Madrid baada ya klabu hiyo kufungiwa kusajili. 
  Mashetani hao Wekundu walimtaka pia mshambuliaji wa Everton, Romelu Lukaku lakini bahati mbaya mchezaji hiyo wa kimataifa wa Ubelgiji ameamua kurejea timu yake ya zamani, Chelsea. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MORATA ASITISHA FUNGATE LAKE SABABU YA MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top