• HABARI MPYA

  Alhamisi, Juni 29, 2017

  MEXIME NA WENGINE 18 WAHITIMU KOZI YA UKOCHA DARAJA A CAF

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA wa Kagera Sugar, Mecky Mexime ni kati ya makocha 19 waliohitimu kozi ya Daraja ‘A’ ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) iliyofanyika Makao Makuu ya Shirikisho la Kabumbu Tanzania (TFF), Uwanja wa Karume, Ilala mjini Dar es Salaam.
  Makocha hao walimaliza gwe ya pili ya siku 19, katika kozi hiyo ambayo mbali ya kuwa na wakufunzi wengine, wakufunzi wakuu wa CAF walikuwa ni Athumani Lubowa na Sunday Kayuni.
  Kayuni ambaye ni Mkurugenzi wa zamani wa TFF katika kozi hii amehudumu kama mkufunzi mkuu wa CAF na aliyekuja kuwasimamia (Accessor) ni Mkurugenzi wa sasa wa Shirikisho la Soka Uganda, Athumani Lubowa.
  Mecky Mexime ni kati ya makocha 19 waliohitimu kozi ya Daraja ‘A’ ya CAF iliyofanyika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam

  Makocha waliohitimu ni Kidao Wilfred Mzigama, Ali Vuai Shein, Wane Nelson Mkisi, Abdulmutik Haji Ali, Hababuu Ali Omar, Meck Maxime Kianga, Salim Ali Haji, Malale Hamsini Keya na Abdallah Mohammed Juma.
  Wengine ni Salim Juma Makame, Emmanuel Raymond Massawe, Mohammed Alawdin Tajdin, Fikiri Elias Mahiza, Juma Ramadhani Mgunda na Dismas Gordon Haonga, Abdul Hassan Banyai, Maka Andrew Mwalwisi, Dennis Mrisho Kitambi na Sebastian Leonard Nkoma.
  Akifunga kozi hiyo, Mgeni rasmi Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa TFF, Khalid Mohammed Abdallah aliwatakia kila la kheri kwa makocha hao akiwaelezea kuwa wamejaa utajiri wa ufundi ambao hawana budi kuutendea haki kwa kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji vya mpira wa miguu.
  Awali, akizungumzia wahitimu hao, Mkufunzi Lubowa alisema kwamba anamini makocha hao watafanya vema kwa kuwa katika kipindi chote cha kozi, walionyesha kuwa na nidhamu ya hali ya juu - alama kuu ya mafanikio.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MEXIME NA WENGINE 18 WAHITIMU KOZI YA UKOCHA DARAJA A CAF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top