• HABARI MPYA

  Ijumaa, Juni 23, 2017

  MOHAMED SALAH ATUA LIVERPOOL KWA DAU LA REKODI

  Mohamed Salah akiwaonyesha vidole gumba wapiga picha kuashiria mambo safi baada ya kukamilisha usajili wake Anfield PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  REKODI ZA WACHEZAJI GHALI LIVERPOOL 

  Mohamed Salah - Pauni Milioni 39 kutoka Roma (Juni 2017)
  Andy Carroll - Pauni Milioni 35 kutoka Newcastle (Januari 2011)
  Sadio Mane - Pauni Milioni 34 kutoka Southampton (Juni 2016) 
  Christian Benteke - £32.5m from Aston Villa (July 2015) 
  Roberto Firmino  - £29m from Hoffenheim (June 2015)
  MSHAMBULIAJI Mohamed Salah amejiunga na klabu ya Liverpool kwa dau la rekodi la Pauni Milioni 39.
  Salah alisafiri kwenda Merseyside Jumanne kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya kuelekea kurejea Ligi Kuu ya England.
  Usajili wa winga huyo wa zamani wa Chelsea umekuwa kipaumbele Liverpool na mazungumzo na klabu yake, AS Roma yalianza tangu mwezi uliopita.
  Klabu hiyo ya Italia ilikataa dau la Pauni Milioni 28 kumuuza Mmisri huyo mwanzoni mwa Juni, lakini makubaliano yamefikiwa kwa sasa na Salah anampiku Andy Carroll kama mchezaji ghali kuwahi kusajiliwa na klabu hiyo.
  Salah, ambaye alipata fursa ya kujiunga na Liverpool miaka mitatu iliyopita, lakini akachagua kuendelea kufanya kazi na Jose Mourinho klabu ya Chelsea, atakuwa analipwa mshahara wa Pauni 90,000 kwa wiki.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MOHAMED SALAH ATUA LIVERPOOL KWA DAU LA REKODI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top