• HABARI MPYA

  Ijumaa, Juni 30, 2017

  MAYWEATHER NA MCGREGOR NI PAMBANO LA 'WAZEE WA MPUNGA'

  KWA kuchanganya utajiri wao, unafika pauni Milioni 288 kwa pamoja.
  Lakini kati ya hizo, Floyd Mayweather ana utajiri wa thamani ya Pauni Milioni 262 na Conor McGregor ana Pauni Milioni 26 tu na wote wafari yao ya kufikia kwenye utajiri na usupa staa huu imeanzia mbali.
  Mayweather, ambaye alisema ameingiza zaidi ya Pauni Milioni 615 katika kipindi chake chote cha kupigana bila kupoteza pambano, safari yake ilianzia kwenye umasikini na kujihusisha na dili za dawa za kulevya katika maghetto huko Grand Rapids, Michigan. 
  Wakati huo huo, McGregor alikuwa bado anahudumiwa nyumbani kwao Dublin hadi mwishoni mwa mwaka 2013.
  Wawili hao watakutana mjini Las Vegas, Marekani mwezi Agosti 26 katika pambano la kihistoria la mapigano baina ya wapiganaji wa michezo tofauti wanaounganishwa kwenye ulingo wa ngumi za kulipwa.
  Ni pambano ambalo linatarajiwa kuingiza zaidi ya Pauni Milioni 467. Lakini je, ni jinsi gani wawili hao walivyotarajika na kuwa maarufu? Tazama picha.

  Floyd 'Money' Mayweather amesema ameingiza zaidi ya Pauni Milioni 615 katika kipindi chake cha kuwa ulingoni PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAYWEATHER NA MCGREGOR NI PAMBANO LA 'WAZEE WA MPUNGA' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top