• HABARI MPYA

  Jumatano, Juni 28, 2017

  MALINZI, MWESIGWA KUPANDISHWA KIZIMBANI LEO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  VIONGOZI wa juu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Rais Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake, Selestine Mwesigwa wanashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa tuhuma ambazo bado hazijajulikana,
  Kwa mujibu wa vyanzo vya Habari kutoka TFF, wakuu hao walichukuliwa jana kwa mahojiano juu ya tuhuma ambazo bado hazijajulikana na huenda leo wakapandishwa Mahakama ya Kisutu.
  “Ni kweli, Rais na Katibu wanashikiliwa kwa mahojiano juu ya tuhuma ambazo hata sisi bado hatujazijua, lakini bado tunaendelea kufuatilia,”kimesema chanzo kutoka TFF.
  Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kulia) akiwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe

  Taarifa zaidi zinasema, wawili hao watapandishwa Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam ambako kama watasomewa mashitaka basi tuhuma zao zitajulikana.
  Na haya yanatokea wakati TFF inaelekea kwenye uchaguzi wake Mkuu, uliopangwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu mjini Dodoma na Malinzi anatetea nafasi yake dhidi ya Imani Madega, Wallace Karia, Fredrick Masolwa, Fredrick Mwakalebela, John Kijumbe, Shija Richard, Ally Mayay na Emmanuel Kimbe.
  Na hiyo ni baada ya mgombea mmoja, Athumani Nyamlani aliyewahi kuwa Makamu wa Rais wa TFF kujitoa.
  Nyamlani aliwasilisha barua ya kujitoa Juni 25, mwaka huu ikiwa ni siku moja tu tangu Kamati ya Uchaguzi ipitishe jina lake kuwa miongoni mwa wagombea 10 wanaowania nafasi hiyo ya urais. 
  Waliojitokeza kuwania Makamu wa Rais na kurejesha fomu wako Mulamu Ng’hambi, Michael Wambura, Geofrey Nyange, Mtemi Ramadhani, Robert Selasela na Stephen Mwakibolwa.
  Ikumbukwe Nyamlani alikuwa Makamu wa Rais wa TFF, chini ya Rais Leodegar Chilla Tenga kati ya Desemba 14, mwaka 2008 na Oktoba 27, mwaka 2013.
  Akawa mpinzani mkuu wa rais wa sasa wa TFF, Jamal Emil Malinzi katika uchaguzi uliopita Oktoba 27, mwaka 2013, lakini akashindwa baada ya kupata kura kura 52 dhidi ya 72 za ‘mbabe wake’.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MALINZI, MWESIGWA KUPANDISHWA KIZIMBANI LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top