• HABARI MPYA

  Ijumaa, Juni 23, 2017

  AKINAA MAMA KIBAO WACHANGAMKIA UCHAGUZI TWFA

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  WANAWAKE wamejitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika Chama cha Mpira wa Miguu Wanawake (TWFA) katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Julai 8, mwaka huu.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TWFA, Msomi Wakili George Mushumba leo Juni 23, aliongoza kikao cha Kamati ya Uchaguzi kupitia majina ya wagombea walioomba kugombea nafasi mbalimbali.
  Mara baada ya kikao hicho, amewataja wanaowania nafasi mbalimbali kwenye mabano kuwa ni Amina Karuma (Nafasi ya Uenyekiti); Rose Kissiwa (Makamu Mwenyekiti); Somoe Ng’itu (Katibu) na Theresia Mung’ong’o (Katibu Msaidizi ).
  Nafasi ya Mweka Hazina, kwa mujibu wa Mushumba inawaniwa na Hilda Masanche ilihali nafasi ya Ujumbe wa Mkutano Mkuu TFF, inawaniwa na Salma Wajesso na Zena Chande huku Ujumbe wa Kamati ya Utendaji TWFA waliopitishwa ni Triphonia Temba, Jasmine Badar, Chichi Mwidege na Mwamvita Kiyogomo.
  Musumba ametangaza majina hayo ya wagombea waliostahili au waliotimiza taratibu za uchaguzi kwa mujibu wa katiba na kanuni za uchaguzi za TWFA. 
  Kinachofuata kwa sasa ni kwamba Juni 26 na 27, 2017- Kupokea pingamizi kati ya saa 4:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni katika ofisi za TFF.

  RATIBA YA UCHAGUZI TWFA
  Juni 28, 2017- Kamati ya Uchaguzi kupitia pingamizi kama zimewasilishwa.
  Juni 29, 2017-  Kamati kutoa majumuisho ya pingamizi kama ziliwasilishwa na wadau. 
  Juni 30, 2017-  Usaili kwa wagombea waliotangazwa.
  Julai 01, 2017- Kutangaza majina ya wagombea waliopitishwa
  Julai 02, 2017-Kamati kupokea rufaa
  Julai 03, 2017-  Kamati kupitia rufaa kama zimewasilishwa.
  Julai 04, 2017   Kamati kutangaza orodha ya mwisho ya wagombea.
  Julai 04 hadi 07, 2017 - Wagombea kufanya kampeni kwa kuzingatia maadili.
  Julai 08, 2017- Uchaguzi Mkuu wa TWFA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AKINAA MAMA KIBAO WACHANGAMKIA UCHAGUZI TWFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top