• HABARI MPYA

  Jumapili, Juni 25, 2017

  UCHAGUZI LIPULI FC SASA KUFANYIKA AGOSTI 5

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imeusogeza mbele uchaguzi klabu ya Lipuli ya Iringa uliopangwa kufanyika Mei 29, mwaka huu ili kupisha taratibu mbalimbali, kanuni na sharia zifanyike kwanza.
  Uamuzi huo umefikiwa baada ya vikao vyake mfululizo vya Juni 10 na 11, mwaka huu, ambavyo pamoja na uchaguzi wa Lipuli vilijadili na mambo mengine pia.
  Uchaguzi huo sasa utafanyika Agosti 5, mwaka huu utasimamiwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kama ilivyopangwa awali na uamuzi huo umezingatia malalamiko yaliyoletwa na wanachama ambao baadhi ya majina yaliyondolewa kwenye daftari la usajili la wanachama.
  Tayari Kamati ya Uchaguzi ya TFF iko Iringa kwa ajili ya kutangaza rasmi uchaguzi huo ambako zoezi la kuchukua na kurejesha fomu litaanza Juni 28, mwaka huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: UCHAGUZI LIPULI FC SASA KUFANYIKA AGOSTI 5 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top