• HABARI MPYA

  Ijumaa, Juni 30, 2017

  WANYAMA KUZURU UGANDA PIA, ATACHEZA HADI MECHI

  KIUNGO wa kimataifa wa Kenya na klabu ya Tottenham Hotspur ya Ligi Kuu ya England, Victor Wanyama atazuru Uganda katika ziara iliyoandaliwa na nyota wa muziki nchini humo, Eddy Kenzo Musuuza.
  Taarifa za vyombo vya Habari zimesema kwamba Musuuza amethibitisha ziara ya Wanyama Uganda itakuwa mwanzoni mwa Julai, mwaka huu.
  Wanyama ambaye msimu uliopita aliiwezesha Spurs kumaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England nyuma ya Chelsea waliotwaa ubingwa, wiki iliyopita alikuwa Tanzania kwa ziara ya aina hiyo pia.
  Na akiwa Uganda, Wanyama anatarajiwa kucheza na mechu ya hisani pia.
  Victor Wanyama alikutana na Mkurugenzi wa Azam TV, Yussuf Bakhresa alipokuwa Tanzania
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WANYAMA KUZURU UGANDA PIA, ATACHEZA HADI MECHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top