• HABARI MPYA

  Jumanne, Juni 27, 2017

  WAINGEREZA WAISHANGAA TANZANIA ILICHOMFANYIA WANYAMA

  Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  VYOMBO mbalimbali vya habari Uingereza vimeonekana kuistajaabu Tanzania kwa kitendo cha kuupa jina la kiungo wa Tottenham Hotspuer mtaa wa Viwanjani na kubatilisha siku moja baadaye.
  Magazeti yote makubwa England yakiwemo The Sun na Daily Mail yameandika kwa mapana marefu habari hiyo na yakimnukuu pia na Wanyama mwenyewe.
  Kwa ujumla Waingereza wanaistaajabu mno Tanzania kwa kitendo hicho, kwani Wanyama ni mchezaji mkubwa ambaye kwa utajiri wake unaotokana na kucheza klabu kubwa England, Spurs akilipwa Pauni 80,000 angeweza kwenda popote kufanya chochote katika mapumziko ya baada ya msimu akachagua kwenda nchi hiyo jirani na kwao.
  Victor Wanyama (kushoto) akiwa Mkurugezi wa Azam TV, Yussuf Bakhresa wiki iliyopita Dar es Salaam

  Ikumbukwe Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Dar es Salaam juzi ilitengua mpango wa kuuita Victor Wanyama uliokuwa mtaa wa Viwandani, eneo la Shekilango, Dar es Salaam, kwa madai jambo hilo lilifanyika kinyume cha utaratibu.
  “Majina ya mitaa hupendekezwa na kamati za mitaa husika kisha hupelekwa kwenye vikao vya WDC vya kata halafu maamuzi ya WDC hupelekwa kwa Mkurugenzi kwa ajili ya kuingizwa kwenye kikao Cha kamati ya Fedha na uongozi, Baraza la Madiwani,”.
  “Halafu DCC,  RCC na Kisha Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na baadaye kwa Mchapaji mkuu wa serikali na mwisho hutokea kwenye Tangazo la serikali GN. 
  Na hapo ndipp mtaa hujulikana huo ni mtaa fulani. Taratibu za kubadili pia lazima zifuate hatua hizo muhimu,” ilisema taarifa hiyo.
  Hatua hiyo ilichukuliwa siko moja tu baada ya kiungo kimataifa wa Kenya, Victor Mugubi Wanyama anayechezea Tottenham Hotspur ya England kupewa heshima hiyo kwa Mtaa wa Viwandani uliopo kata ya Shekilango, Manispaa ya Ubungo kupewa jina lake.
  Na hiyo ilifuatia ziara ya kiungo huyo wa klabu ya Tottenham Hotspur ya England nchini kwenye Uwanja wa Kinesi, uliopo eneo hilo kushuhudia mechi za mashindano madogo. 
  Baada ya kupewa Mtaa huo, Wanyama alisema; “Nitoe Shukrani zangu za dhati kwa Meya na wakazi wote wa Manispaa ya Ubungo kwa kunikaribisha na kulipatia jina langu barabara ya mtaa wa NHC. Naahidi kurudi tena na Ahsanteni sana kwa ukarimu na makaribisho mlionipa. Asante Tanzania,”.
  Lakini baada ya mabadiliko hayo, Wanyama akasema amesikia Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda ameagiza mpango huo usitishwe kwanza hadi taratibu zifuatwe na akampe pole Meya wa Ubungo,”.
  Kihistoria, Wanyama aliyezaliwa Juni 25, mwaka 1991 alisoma shule ya Kamukunji  na kisoka aliibukia akademi ya JMJ kwao, kabla ya kuchezea klabu za Nairobi City Stars na AFC Leopards katika Ligi Kuu ya Kenya.
  Mwaka 2007 alijiunga na Allsvenskan ya Helsingborg nchini Sweden, lakini akalazimika kuondoka baada ya kaka yake, McDonald Mariga kwenda Parma ya Italia mwaka 2008 na Wanyama akarejea Kenya.
  Baadaye akaenda kufanya majaribio Beerschot AC ya Ubelgiji na kufuzu, hivyo kusaini mkataba wa miaka wa minne kuanza kucheza rasmi Ulaya mwaka 2008, kabla ya mwaka 2011 kununuliwa na Celtic ya Ligi Kuu ya Scotland.
  Mwaka 2013 alinunuliwa na Southampton ya England kwa dau la Pauni Milioni 12.5 na kuwa Mkenya wa kwanza kucheza Ligi Kuu ya England. Baada ya mechi 85 akifunga mabao manne, Wanyama akanunuliwa na Tottenham Hotspur mwaka jana kwa dau la Pauni Milioni 11 na msimu huu ameiwezesha timu hiyo kumaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu, nyuma ya Chelsea walioibuka mabingwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WAINGEREZA WAISHANGAA TANZANIA ILICHOMFANYIA WANYAMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top